MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'ARSHI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARSHI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARSHI'

Neno *arshi*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Kiti kitukufu cha ufalme na utukufu wote wa Mwenyezi Mungu; kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu.

2. Kiti cha uongozi cha Mfalme, Rais au mtawala mwengine; kiti cha mamlaka.

3. Malipo anayotoa mtu kama fidia kwa kumsababishia mtu mwengine kutoka damu au kifo cha mtu.

Neno *arshi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *arshu* ( *soma: arshun/arshan /arshin عرش )*  neno lenye maana zifuatazo:

1. Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu.

2. Ufalme, utawala.

3. Kiti cha enzi/kitanda cha mfalme.

4. Dari ya nyumba.

5. Paa la nyumba aghalabu lililotengenezwa kwa matete,  mwamvuli mkubwa.

6. Miti inayofungwa kwenye mizabibu ili kuisimamisha.

7. Kiongozi wa kundi la watu *arshul qawmi عرش القوم.*

8. Kiota cha ndege  *arshutw twaairi عرش الطائر.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *arshu عرش* lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *arshi* halikubadili maana zake za kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, kiti cha enzi cha mtawala (rais, mfalme) na mamlaka na ufalme bali liliacha maana zingine katika Kiarabu na kuchukua maana mpya ya fidia inayolipwa kwa kusababisha mtu kutokwa damu au kifo cha mtu.

Neno la Kiarabu lenye maana ya fidia inayolipwa kwa kusababisha mtu kutokwa damu au kifo cha mtu ni *diyah (soma: diyatun/diyatan/diyatin  دية).*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*