MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUFU''

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUFU''
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUFU''

Neno arufu  katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya nywele ndefu zinazoota kuzunguka shingo ya mnyama kama vile simba, farasi.

Neno arufu limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu urfu ( soma: urfun/urfan /urfin عرف )  neno lenye maana zifuatazo:

1. Tabia za jamii, desturi.

2. Jambo maarufu lililozoeleka kufanywa na jamii fulani.

3. Nywele za shingoni mwa farasi.

4. Upanga wa jogoo.

5. Sehemu ya ardhi iliyoinuka.

6. Kilele cha mlima.

7. Wimbi la bahari. 

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  urfun عرف lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno arufu lilichukua kutoka Kiarabu maana mahsusi ya nywele ndefu zinazoota kuzunguka shingo ya farasi na kuifanya maana ya nywele ndefu zinazoota kuzunguka shingo ya mnyama kama vile simba na farasi.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.