MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'ALJEBRA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'ALJEBRA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ALJEBRA''

Neno *aljebra*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/i-]* yenye maana ya tawi la hisabati ambamo herufi na alama hutumika kuwakilisha idadi fulani.

Neno *aljebra* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *aljabru* ( *soma: aljabru/aljabra/aljabri الجبر)*  lenye maana zifuatazo:

1. Istilahi ya Sharia ya Kiislamu yenye maana ya uchaguzi mbaya aufanyao mwanadamu katika vitendo vyake; *al-ikraah الإكراه.*

2. Istilahi ya Sharia ya Kiislamu yenye maana ya kukamilisha.

3. Tawi mojawapo la hisabati pamoja na nadharia ya namba, jiometri na uchambuzi.

4. Kuunga kilichovunjika kama vile mfupa.

5. Kutengeneza jambo na kuliimarisha.

6. Kumlazimisha mtu kufanya kitendo fulani.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *aljabru الجبر* lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *aljebra* lilichukua kutoka Kiarabu maana ya *tawi mojawapo la hisabati* na kuacha maana zingine.

*TANBIHI:*
Neno hili *aljabru  الجبر* ( *aljebra* ) ni istilahi ya tawi la hisabati linalotumia ishara kutatua matatizo ya hisabati.

Katika muundo wake wa kiujumla *aljabru (aljebra)* ni somo la ishara za kihisabati na sheria za kuendesha ishara hizo; ni uzi unaounganisha karibu matawi yote ya hisabati ikijumuisha kila kitu kutoka kwenye misingi ya kutatua milinganyo.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*