MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIHAMI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIHAMI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARIHAMI'

Neno *arihami* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: a-/-wa*] yenye maana ya *ndugu wa upande wa mwanamke.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *arihami* limechukuliwa na kutoholewa kutoka neno la Kiarabu *arhaam* ( *soma: arhaamun/arhaaman/arhaamin ارحام )* lililo wingi wa neno la Kiarabu *Rahim (soma: rahimun/rahiman/rahimin  رحم)* lenye maana ya *mji wa uzazi.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno *arhaamun ارحام*  huwa linaanza na *dhuu ذو* na kuwa *dhul arhaami ذو الأرحام* lenye maana ya *wenye ujamaa/udugu; ndugu wa karibu* .

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *arhaamun ارحام* lilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *arihami* liliacha maana ya jumla ya wenye ujamaa/udugu; ndugu wa karibu katika lugha asili - Kiarabu na kuchukua maana mpya ya ndugu wa upande wa mwanamke.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*