MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANA'

Neno *amana*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Kitu anachokabidhiwa mtu kwa utaratibu maalumu ili akihifadhi kwa muda na kukirejesha kwa mmiliki kitakapohitajika.

2. Kiasi cha fedha kilichowekwa benki; *akiba* .

3. Kitu chenye thamani kubwa.

Katika lugha ya Kiarabu neno *amana* linatokana na neno la Kiarabu *amaanah (soma: amaanatun/amaanatan/amaanatin  امانة)* lenye maana  zifuatazo:

1. Kusalimika, nomino inayotokana na kitenzi cha Kiarabu *amina  امن* amesalimika.

2. Akiba.

3. Hali ya kuhifadhi upendo na kutekeleza ahadi kwa namna inavyopasa.

4. Alichokifaradhisha (alichokifanya lazima/wajibu) Mwenyeezi Mungu kwa watu.

5. Msimamo thabiti na ukweli.

6. Chombo cha uendeshaji na usimamizi wa shughuli za taasisi, chama, jumuiya *al-amaanatul aamah الأمانة العامة* ofisi ya Katibu Mkuu; *Sekretarieti*.

7. Mamlaka ya usimamizi wa mji mkuu, *amaanatul aaswimah عاصمة العاصمة.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno *amaanatun امانة*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *amana* lilichukua baadhi ya maana za neno hili katika lugha asili - Kiarabu na kuyaacha mengine.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*