MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'ITIFAKI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'ITIFAKI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ITIFAKI'

Neno *itifaki*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Maafikiano baina ya pande mbili kuhusu jambo fulani; *maelewano, maridhiano.*

2. Taratibu za kiserikali kushughulikia na kuhudumia shughuli rasmi za viongozi na utawala; *protokali* .

*Mfano* : Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imezungumzia uanzishwaji wa Kamisheni ya Kiswahili.

Katika lugha ya Kiarabu neno *itifaki* linatokana na neno la Kiarabu *ittifaaq (soma: ittifaaqun/ittifaaqan/ittifaaqin  اتفاق)* lenye maana  zifuatazo:

1. Maelewano au mapatano baina ya nchi mbili ya kumaliza mzozo.

2. Maafikiano baina ya pande mbili kuhusu jambo fulani; *mkataba*.

3. Hali ambapo mambo au matukio mawili au zaidi hutokea kwa wakati mmoja bila ya kupangwa au kutarajiwa; *sadfa*.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *ittifaaq اتفاق*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *itifaki* maana ya *mapatano; mkataba* haikubadilika bali Waswahili waliongeza maana ya *protokali* ambapo Waarabu hutumia neno ' *maraasimu* ' ( *soma: maraasimu/maraasima مراسم)*.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*