MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'ANUANI/ANWANI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'ANUANI/ANWANI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ANUANI/ANWANI'

Neno *anuani/anwani*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Maelezo ya mahali ambapo mtu huishi au hufanya kazi, ambayo husaidia kumfikishia kufurushi au barua iliyotumwa hasa kwa njia ya posta; mahali panapotumiwa kufikishia barua.

2. Akaunti ya mtandao wa kutuma na kupokea barua kupitia mfumo wa intaneti.

3. Mada au jina la kitabu.

Katika lugha ya Kiarabu neno *anuani/anwani* linatokana na neno la Kiarabu  *unwaaanu (soma: unwaanun/unwaanan/unwaanin عنوان)* lenye maana  zifuatazo:

1. Kinachotoa utambulisho wa kipekee kwa kitu usiofanana na mwengine. Kwa mfano: *Unwaanul Kitaabi  عنوان الكتاب* anuani ya kitabu.

2. Maandishi yaliyodhihirishwa yanayoelezea kilichofichwa.

3. Maandishi yanayoandikwa juu ya bahasha kubainisha anayepelekewa na makazi yake.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *unwaanun  عنوان*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *anuani/anwani* maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu inayohusu utambulisho haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*