MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'ANSARI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'ANSARI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ANSARI'

Neno ansari  katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: a-/wa-] yenye maana zifuatazo:

1. Wakazi wa mji wa Yathribu (sasa Al-Madiinatu Al-Munawwarah/Madina) waliwapokea Muhajirina (Waislamu waliouhama mji wa Makkah) na Mtume Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani) na wakawanusuru na kumuunga mkono Mtume Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani) dhidi ya maadui zake Maqureishi Washirikina wa Makkah.

2. Kundi la watu wanaoenzi na kunusuru matendo aliyoyafanya Mtume Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani).

Ansari Sunna; Wafuasi wa matendo ya Mtume Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani).

3. Waokoaji.

Katika lugha ya Kiarabu neno ansari linatokana na neno la Kiarabu  answaaru (soma: answaarun/answaaran/answaarin أنصار) lililo wingi wa neno naaswirun ناصر lenye maana  zifuatazo:

1. Al-Answaaru; watu wa mji wa Yathribu (sasa: Madina) waliomhami Mtume Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani) kutokana na maadui zake wa mji wa Makkah na wengineo.

2. AN-NAASWIRU الناصر, Mwenye kunusuru, moja ya majina matukufu ya Mwenyeezi  Mungu.

3. Naswiirun ناصر, jina la mwezi wa 6 (Juni) kwa Kalenda ya nchi ya Libya.

Kinachodhihiri ni kuwa neno answaarun  انصار  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno ansari maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu inayohusu watu wa Madina na watu wenye kunusuru; waokoaji haikubalika.

TANBIHI:
Mambo yafuatayo ni ya kuzingatiwa:

1. Ansari ni wanaoenzi, kunusuru na kufuata Sunna (mambo yote yaliyohusishwa na Mtume Muhammad - Allaah Amrehemu na Ampe Amani -  iwe kauli yake, kitendo chake au lile alilolikubali lilipofanywa mbele yake) na sio matendo yake tu.

2. Katika kujipambanua, Libya chini ya Kiongozi wake wa zamani Marehemu Muammar Gaddafi, ilibuni na kuanzisha majina ya miezi tofauti na wengine na wakati mwaka wa Kalenda ya Ulimwengu wa Kiislamu unaanzia toka kuhama kwa Mtume  Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani) kutoka Makkah na kuhamia Madina, Libya ilihesabu Kalenda yake toka kutawafu kwa Mtume  Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani).

3. Jina Naaswirus Sunnah, mwenye kunusuru Sunnah au Answaarus Sunnah, wenye kunusuru Sunna ni jina kongwe walilojinasibisha nalo baadhi  ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Karne nyingi zilizopita.

Jina hili lilipata umashuhuri zaidi lilipotumiwa na wafuasi  wa  Mwanazuoni Sheikh Muhammad Abdul-Wahabi (Allaah Amrehemu) katika kinachoitwa mwamko mpya wa Uislamu.

Wafuasi hawa wametambulika kwa majina mengi kama vile: Mawahabi (jina linalotumiwa sana na wapinzani wao), Masalafi, Ahlus Sunnati Waljamaa, Salafi Jadiid na mengineyo.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.