MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHRAFU'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHRAFU'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHRAFU' 

Neno *bashrafu*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya *muziki unaopigwa kwa ala tupu bila ya maneno.*

Katika lugha ya Kiarabu neno *bashrafu* linatokana na neno la Kiarabu  *bashrafu (soma: bashrafun/bashrafan/bashrafin بشرف)* lenye maana ya *utangulizi wa muziki unaopigwa kwa ala tupu bila ya maneno.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno *bashrafun  بشرف*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *bashrafu* maana yake ya msingi katika lugha ya Kiarabu haikubadilika.

*TANBIHI:*
Ingawa Waswahili wamesajili etimolojia ya neno hili *bashrafu* kuwa Kiarabu, uchunguzi wa asili ya maneno umebaini kuwa neno hili etimolojia yake ni *Kifursi/Kiajemi* na Waarabu wamelichukua huko.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*