MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: NANI ATAKUWA WAO?

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: NANI ATAKUWA WAO?
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Hongera Sana kwa shairi hili zuri! Mungu akujalie zaidi!
NANI ATAKUWA WAO?

Ninaona magalacha, wa lugha ya Kiswahili,
Umri unawaacha, si kama vile awali,
Ni Nani wamemuacha, kukitunza Kiswahili,
Nani awe Mlokozi, akipokeze kijiti.

Viti Sasa waviacha, ni vitupu yake hali,
Nawaza usiku kucha, vile nafikiri mbali,
Usia hawajaacha, waseme lile na hili,
Nacho kiti cha Kahigi,  nani atakikalia?

Mfano wa Mtembei, yu wapi nawauliza?
Aje hapa ajidai, kuwa kazi aiweza,
Hata mie simjui, nani atampokeza,
Nani atwambie wazi, mrithi wa huyu nguli?

Bado napata kihoro, mambo haya nikiona,
Ninani awe Senkoro, aandike kwa mapana,
Naona kuna kasoro, nikiwaona vijana,
Nani ajitaje jina, Kiswahili kukikuza.

Nimesikia Massamba, umri umekimbia,
Japo lugha alipamba, mfano Fonolojia,
Naona twaenda yumba, sioni wakufidia,
Leo nani atatamba, aseme ndiye Massamba.

Kwa mtu kuwa mahiri,  kuacha aseme mwiko,
Aishike Tafsiri, amkaimu Mwansoko,
Leo niwambie siri, mpaka Sasa hayuko,
Mrithi wake Mwansoko, hayupo zamani hizi.

Bado napata mashaka, mambo haya takuaje,
Mana nafanya haraka, kuandika nisingoje,
Japo wakati nachoka, neno hili nisitaje,
Nikipoleze kijiti, na chini kisidondoke.

Nikimuona Penina, ametingwa siku hizi,
Najua na muda hana, kuandika zake kazi,
Kuna pengo naliona,
Ukweli mekuwa wazi,
Aandike nguzo mama, ningali bado kumwona.

Sasa ninalia ngoa, tunusuru Kiswahili,
Wale tunotegemea, wapumzishe akili,
Zamu yetu kuilea, hii lugha Kiswahili,
Tusimameni vijana, tuandike kwa awamu.

Limelia la mgambo, amkeni amkeni,
Kiswahili ndio Jambo, lugha tuiandikeni,
tusijefata mikumbo, eti ni ya kazi gani,
Mkana kwao mtumwa, amini habari hizi.

Nimewapa mfahamu, kuna hili hitajio,
Ni changa zetu fahamu, tuandike kwa vituo,
Mwisho tuwe maalimu, tuzifanye kazi zao,
Kijiti cha magalacha, kamwe sidondoke chini.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Ujumbe mzuri kabisa