MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AFUENI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFUENI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
*HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFUENI'.*

Neno *afueni* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/i-]* yenye maana zifuatazo:

1. Hali nzuri ya afya inayomrejea mtu baada ya kuugua au kuwa katika maumivu.

2. Unafuu aupatao mtu baada ya kuondokewa au kupungukiwa na ugumu au uzito wa jambo; nafuu.

3. Tendo la kupungua kwa maradhi, hali ya kupata hujambo.

*Nahau*: *pata afueni:* pata nafuu.

Kamusi Kuu ya Kiswahili imetoa fasili ya neno hili kwa  kuandika: *tazama ahueni.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno *afueni* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *afwan*( *soma: afwun/afwan/afwin عفو)*, nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Wema, ubora.

2. Ziada ya mali isiyomsumbua mwenye mali kuitoa.

3. Msamaha kama ule anaoutoa raisi wa nchi kwa wafungwa.

4. Tamko la kuomba msamaha; *afwan! عفوا* samahani.

5. Kufanya jambo, kama vile kutoa hotuba, bila ya kujiandaa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *afwan  عفوا* lilipoingia katika Kiswahili  na kutoholewa kuwa neno *afueni* limefanywa *kisawe* cha neno *ahueni* na kuacha maana zake katika lugha asili - Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*