MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: MWENDANI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: MWENDANI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MWENDANI

1. Mwendani wako mwendani, ukitaka umjuwe
Ngia naye safarini, mwenende mwendo wa kuwe
Au muate nyumbani, ukatembee ukawe
Akosapo kuwa mwewe, huyo ni wako mwendani

2. Mwendani wako mwendani, ukitaka mjuato
Mpishe ndia zenye mwani, zenye miba na tototo
Au mbwagie zani, ambayo kwamba ni nzito
Akuonyapo mapito, huyo ni wako mwendani

3. Mwendani wako mwendani, ukitaka mfeeli
Moyowo utie kani, utumie yakwe mali
Umuonapo haneni, hakuregeza kauli
Hashabihi hamithili, huyo ni wako mwendani

- Muyaka bin Haji (mshairi wa Mombasa, aliyeishi baina ya mwaka 1776 na 1840).

*mwenende- mwende
*mwendo wa kuwe - mwendo mrefu; masafa marefu
*muate - mwache
*ukawe - uchelewe
*akosapo kuwa mwewe - asipokunyakulia/asipokuibia chako
*ukitaka mjuato - ukitaka kumjua vizuri
*mpishe ndia - mpitishe njia
*tototo - tope
*mbwagie zani - mwangushie balaa; mpe tatizo kubwa
*akuonyapo mapito - akikuonesha njia za kupita (ili kutoka kwenye tatizo hilo)
*ukitaka mfeeli - ukitaka kumtenda/kumjaribu
*moyowo - moyo wako
*hakuregeza kauli - hakusema neno; hakulalamika
*hashabihi hamithili - hakutoa hata ishara ya kulalamika au kukasirika