MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'USHIRIKINA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'USHIRIKINA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'USHIRIKINA'

Neno *ushirikina* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino [Ngeli: u-/u-]* tabia ya mtu kuamini katika mambo ya uchawi.

2. *Nomino [Ngeli: u-/u-]* tabia ya kuamini mambo ya ramli na uchawi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ushirikina* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *mush-rikiina* *wenye kufanya shirki ( *soma: shirkun/shirkan/shirkin شرك)*  nomino ya Kiarabu  yenye maana zifuatazo:

1. Fungu; kasma; sehemu ya kitu. *Haadha shirku-hu هذا شركه* hili ni fungu lake.

2. Itikadi ya kuamini *uwepo wa miungu wengi.*

Wanazuoni wa Kiislamu akiwemo Imam Shaukany wameibainisha *shirk (ushirikina)* kuwa ni kumuomba asiyekuwa Mwenyeezi Mungu mambo yanayomuhusu Mwenyeezi Mungu Pekee, kuamini uwezo wa asiye kuwa Mwenyeezi Mungu katika mambo asiyoyaweza yeyote isipokuwa Yeye Mwenyeezi Mungu na kujikurubisha kwa asiyekuwa Mwenyeezi Mungu kwa mambo ambayo hapaswi mtu kujikurubisha isipokuwa kwa Mwenyeezi Mungu Pekee.

Sheikh Sulaiman bin Abdillaah Aali Sheikh ameibainisha ' *Shirki' (Usirikina)* kuwa ni kumfananisha kiumbe na Mwenyeezi Mungu Muumba katika mambo mahsusi ya Mwenyeezi Mungu Pekee kama kumiliki madhara na manufaa, kutoa na kuzuia, na kumuabudu asiyekuwa Mwenyeezi Mungu.

Kinachodhihiri ni kuwa maneno ya Kiarabu *mushrikiina na shirki مشركين/شرك)*  yalipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno  *ushirikina* yalipewa maana mpya: *tabia ya kuamini mambo ya ramli na uchawi* na kuiacha maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*