MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI'

Neno *akisami* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Sehemu ya kitu, umbo au tarakimu kama vile robo (1/4), theluthi (1/3), au nusu (1/2).

2. Umbo au namba isiyo kamili.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *aksami*( *soma: aqsaamun/aqsaaman/aqsaamin اقسام)*  ni nomino ya Kiarabu, wingi wa neno la Kiarabu *qismun قسم* lenye maana ya fungu au sehemu ya kitu kilichogawanywa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *aqsaamun/aqsaaman/aqsaamin أقسام)*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno  *aksami* maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*