MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'SADFA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'SADFA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'SADFA'

Neno sadfa katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya hali ambapo mambo au matukio mawili au zaidi hutokea kwa wakati mmoja bila ya kupangwa au kutarajiwa .

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili sadfa( soma: swidfatun/swidfatan/swidfatin صدفة ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana ya kukutana bila ya kukubaliana au kuwa na miadi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili swidfatun/swidfatan/swidfatin صدفة lilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' sadfa ' halikubadili maana ya lugha asili - Kiarabu ya kutokea jambo au tukio bila ya kupangwa.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.