MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AFRO

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFRO
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFRO'

Neno *afro* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Kivumishi* : -enye asili ya Afrika; -a Kiafrika.

2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* mtindo wa ufugaji wa nywele ndefu aghalabu za Kiafrika na kuzitengeneza kuwa katika umbo la kititamviringo kinachofungamana kichwa kizima. 

Ingawa *Kamusi Kuu ya Kiswahili* limelisajili neno hili *afro* kuwa etimolojia yake ni *Kiarabu* lakini *utafiti* nilioufanya umeonesha kuwa neno hili *(afro) si neno la Kiarabu.*

Neno lenye mzizi unaoshabihiana na neno hili ni neno *frau* *فرو* lenye maana ya ngozi za wanyama zinazotumika kutengeneza nguo za kujikinga na baridi.

Yapo madai kuwa neno *afro* lina asili ya *Kilatini* na wengine wamedai kuwa etimolojia yake ni *Kiingereza* .

*Kinachodhihiri ni kuwa neno (afro) halina uhusiano na lugha ya Kiarabu.*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*