MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI'

Neno *afyuni* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli:i-/i-]* yenye maana ya 'kileo chenye umbo la kidonge kunachotengenezwa kutokana na utomvu wa *mpopi*( *afyuni* ) , ambacho kwa kawaida hutumika kama tiba ya kutuliza maumivu, aghalabu hutumiwa kinyume cha sheria kama dawa  ya kulevya.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afyuni* (soma: *afyuunun/afyuunan/afyuunib افيون)* lina maana ya 'dutu inayotolewa kwenye mpopi (afyuni) ambayo inatia ganzi na hutumiwa kwa kutuliza maumivu na kuleta usingizi, pia hutumika vibaya kama dawa ya kulevya.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *afyuni* ( *soma: afyuunun/afyuunan/afyuunin افيون*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *afyuni* halikubadili maana yake ya msingi katika  lugha ya asili - Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*