MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI : KA’NINGAKUWA RAISI, NINGESHITUWA DUNIYA

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI : KA’NINGAKUWA RAISI, NINGESHITUWA DUNIYA
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
SHAIRI : KA’NINGAKUWA RAISI, NINGESHITUWA DUNIYA
Raisi ningalikuwa, wa nchi ya Waswahili,
ninajisikia kuwa, ningetowa yangu kali,
wangu ulimi nikawa, nanena kula pahali,
na n’kifika Marekani, hotuba kwa Kiswahili.
*****
Kwa Wachina nikienda, ninawamba Kiswahili,
kwa Warusi nikipanda, nao wafahamu hili,
kula ya duniya kanda, n’getumia Kiswahili,
wakalimani wakawa, wanafasiri hotuba.
*****
Ningelonga kwa sitaha, na ufahari jameni,
ugenini wakahaha, maso wakakodoeni,
ino lugha ya madaha, n’geiwamba kwa makini,
waelewe Afirika, nasi tunao ulimi.
*****
Taswira itafakari, Ureno nimewasili,
mabingwa wanahabari, wafuatia Kiswahili,
ino ni lugha ya kheri, ‘ngefana kula pahali,
ka’ningakuwa Raisi, ningeshituwa duniya.
*******

Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.