MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI : WAMAMA WA KAMBO WEMA

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI : WAMAMA WA KAMBO WEMA
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
SHAIRI : WAMAMA WA KAMBO WEMA
************
1. Ipo dhana kwao wengi,
mbaya mama wa kambo,
habari hizi ni nyingi,
siamini haya mambo.

2. Nina ushuhuda mwingi,
wa kuthubutu kusema,
wapo wa upendo mwingi,
wamama wa kambo wema.

3. Nilipata kuyaona,
mnyambi haswa mzazi,
‘kimchoma wake mwana,
kisa eti ni andazi.

4. Unapoijenga dhana,
kuwa mtu ni mbaya,
unamchochea sana,
kukufanyia ubaya.

5. Unapoijenga dhana,
kuwa mtu ni mzuri,
unamchochea sana,
kukufanyia mazuri.

6. Jameni mama wa kambo,
mlezi aso hiyana,
anafanya mema mambo,
ukimthamini mwana.

*******
Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.