MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI : KUELIMIKA NI KUPI?

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI : KUELIMIKA NI KUPI?
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
SHAIRI : KUELIMIKA NI KUPI?
1.
Ipo dhana kwao wengi, yahusu ”kuelimika”,
kuwa ni darasa nyingi, unopita mingi ‘miaka.
Tangu shule ya msingi, hadi upili kufika,
ukenda chuo kikuu, eti umeelimika.
2.
Jamii inakulola, kuwa weye mwelekezi,
mengi yao masuala, utayapigia mbizi.
Watu wanakuchagula, kuwa wao kiongozi,
kisa umeelimika, mwana wao ‘tawafaa.
3.
Eti umeelimika, mzito wajisikia,
wajifanya mtukuka, msomi wa kuzamia.
Maarifa uloweka, mwalimu kakupakia,
ubongo ulipojaza, eti umeelimika.
4.
Ulisoma falsafa, sana ukaikariri,
ukiitwa filosofa, wajisikia mahiri.
Matokeoye mshefa, wajifanya ntoka mbali,
unaujenga ukuta, katiyo na jamiiyo.
5.
Yote uliyakariri, ulotafiti hakuna,
hata moja ninakiri, ulovumbua hapana.
Angalau ‘ngefikiri, kuwa wa nyumbani mwana,
ma’rifa ulokusanya, yakawafaa jamaawo.
6.
Ni kupi kuelimika, wanakwetu washairi?
tungeni yakutungika, nyi wasanii mahiri.
Wale waloelimika, na kujifanya hatari,
wapeni ma’na halisi, ”kuelimika ni kupi?”
______

Rwaka rwa Kagarama,(Mshairi Mnyarwanda)
Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare,
RWANDA.- rwakakagarama2020@gmail.com