MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: MWAKA MPYA, JIPANGE UPYA

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: MWAKA MPYA, JIPANGE UPYA
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MWAKA MPYA, JIPANGE UPYA

Mwalimu ametwambia, Lupogo ametamka,
Mwaka unapofikia, upya Simama hakika,
Kaa ukifikiria, jiandae na zinduka,
*Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.*

Upya jikazeĀ  sikia, jitahidi chakarika,
Jua palipo na nia, pambana njia kushika,
Kazana na pangilia, malengo utayafika,
*Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.*

Lima na wako dhuria, tumia zana husika,
Lima kilimo huria, cha matunda na nafaka,
Lima ukimwagilia, na mbolea ukiweka,
*Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.*

Tafuta na ulizia, masoko ya uhakika,
Chambua na fikiria, amua la muafaka,
Sitanie ukalia, usiujaribu mwaka,
*Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.*

Tingisha na shikilia, jieleze na sikika,
Imba wasije kimbia, burudani wanataka,
Cheza mpira, kimbia, jiongeze huu mwaka,
*Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.*

Tama hapa naishia, ya Lupogo kuandika,
Kwa ushairi jadiya, masivina sikutaka,
Heri ninawatakia, ya shari kuwaepuka,
*Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.*

*Khamis S.M. Mataka*
*Dar es Salaam, 31.12.2021*