MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI'

Neno *afiriti*[ *Ngeli: a-/wa-]* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: ya:

1. Mtu anayechochea wenzake kufanya maovu.

2. Shetani aletaye madhara kwa watu, maluuni, jini, ibilisi.

3. Mtu mwenye tabia za ujanjaujanja, mdangayifu.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afiriti* (soma: *ifriit عفريت)* ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mtu khabithi/habithi, muovu, mdaganyifu.

2. Mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu katika kutenda jambo fulani; mahiri.

3. Jini, shetani, pepo.

4. Kreni inayoinua magari na kadhalika.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *afiriti* ( *soma: ifriit  عفريت*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *afiriti* maana zake zinazohusu jini na mtu mjanjamjanja/mdanganyifu hazikubadilika isipokuwa limeacha maana zingine katika Kiarabu na kuchukua dhana ya mtu anayechochea wenzake kufanya maovu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*