MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA MANENO ' ABSARI' na 'ABUNUWASI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA MANENO ' ABSARI' na 'ABUNUWASI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' ABSARI' na 'ABUNUWASI'

Neno *Absari* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino* yenye maana ya hali ya kung'amua jambo fulani.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *absara* ( soma: *abswara*  *(أبصر)* ni kitenzi chenye maana ya:
1. Ameona kwa mbali.

2. Ameng'amua kitu kwa mbali na kwa uwazi kabisa.

Na neno *Abunuwasi* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana ya 'muhusika katika hadithi  za masimulizi yenye asili ya Kiarabu, ambaye aghalabu huibuka kuwa mshindi katika matukio mbalimbali  kutokana na ujanja wake, kama alivyo Sungura katika masimulizi yenye asili ya Kiafrika.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *abunuwasi* ( soma: *Abuu Nuwwaas * *ابو نواس* ) ni jina la kipekee la al-Hasan  ibn Hani ibn al-Hakami, (Alizaliwa katika eneo la Ahvaz, nchini Iran, mwaka 756 na kufariki katika mji wa Baghdad, Iraq mwaka 814) mshairi nguli na nguzo ya Ushairi wa Kiarabu wa Kisasa ulioibuka mwaka wa kwanza wa ukhalifa wa Abasiyya/Abbasid - Abbasid Caliphate (Utawala wa Kiislam katika Mashariki ya Kati kutoka karne ya 8 hadi karne ya 13.)

Pia Abuu Nuwwaas alijiingiza katika utunzi wa Hadithi za masimulizi ya jadi na anajitokeza mara kadhaa katika Hadithi ya masimulizi ya Alfu Leila Uleila (Nyusiku/Siku Elfu Moja na Usiku mmoja.)

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *abswara* *ابصر*) ambalo ni kitenzi cha Kiarabu lilipoingia katika lugha ya Kiswahili lilibadilika kuwa *nomino* ingawa maana ya kuona na kung'amua haikubadilika.

Kadhalika, neno *abunuwasi* ambalo limeingia katika Kiswahili kama muhusika wa  Hadithi za masimulizi yenye asili ya Kiarabu, kiasili ni jina la mtu aliyekuwa nguli katika ushairi na hadithi za masimulizi ambaye mtindo wa masimulizi yake ni kujieleza yeye mwenyewe jambo lililomtangaza zaidi kwa sifa ya muhusika wa masimilizi hayo kuliko kuwa ni mtunzi wa masimulizi hayo.

*NYONGEZA YA MAKALA KUHUSU ETIMOLOJIA YA NENO ABUNUWASI.*

Baadhi ya wapenzi wasomaji wa *makala za Etimolojia* wameomba maana ya neno ' *nuwasi* ' kama lilivyodhihiri katika neno ' *abunuwasi* '.

Neno ' *nuwasi* ' ni nomino ya Kiarabu ' *nuwwaas* ' (soma: *nuwwaasun/nuwwaasan/nuwwaasin نواس* ) na maana yake kwa Kiswahili ni *tandabui* (utando ambao hutengenezwa na buibui).

Katika lugha ya Kiarabu pia neno hili hujumuisha *utandu unaotengenezwa darini kutokana na moshi au vumbi.* 

Hivyo basi, Abunuwasi (Abuu Nuwwaas) maana yake ni *baba wa tandabui.*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*