MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA MANENO 'ABIRI' na 'ABIRIA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA MANENO 'ABIRI' na 'ABIRIA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'ABIRI' na 'ABIRIA'

Neno abiri katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino* : Harufu nzuri inayonukia; manukato ya kupendeza.

2. *Kitenzi elekezi:*
(i) fafanua jambo kwa vizuri, (ii) eleza jambo litakavyojiri; tabiri.

3. *Kitenzi si elekezi:*
(i) safiri kutoka eneo moja kwenda jingine kwa kutumia chombo chochote cha usafiri.
(ii) fanya safari kwa chombo cha majini.

4. *Kitenzi si elekezi:* elimika na jambo kwa kutumia mfano uliokwishatokea. (Visawe: tahadhari; jihadhari; kuwa mwangalifu.)

5. *Kitenzi si elekezi:* ingia katika chombo cha kusafiri, kwa mfano, meli, basi, mashua na kadhalika.

Neno *abiria* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino* yenye maana ya: mtu anayetoka mahali fulani na kwenda pengine kwa kutumia chombo kwa mfano, basi, treni na kadhalika na ambaye si mfanyakazi wa chombo hicho.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *abiri* limetokana na vitenzi vya Kiarabu *abara* *عبر*  na pia *abbara* *عبر* vyenye maana zifuatazo:

1. Amevuka (barabara au mto).

2. Amesafiri na chombo cha majini.

3. Amekufa/Amefariki/Ametawafu.

4. Amepita/Yamepita.

5. Ameieleza vyema habari fulani.

6. Amefasiri ndoto. 

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *abara* *عبر*) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *abiri* , maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika ingawa lilichukua baadhi za maana na kuacha maana zingine.

Ama neno *abiria* , hili si neno halisi la Kiarabu bali ni matokeo ya usanifishaji na unyambulishaji wa neno *abiri* kutoka neno la Kiarabu *abara/abbara.*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*