MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - KISA CHA MVUVI NA SAMAKI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: KISA CHA MVUVI NA SAMAKI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Mfalme alipata hamu ya kula samaki akaamua kutembelea ufukweni siku hiyo ikawa samaki hakuna wavuvi wote wamekosa samaki
Wakati anarudi na wafuasi wake ndipo akakutana na Mvuvi mmoja tu alie bahatika kupata samaki watatu 3 Mfalme akataka kuwanunua Mvuvi akakataa kuwauza samaki wake.

Mfalme akaomba auziwe japo mmoja Mvuvi akamwambia Mfalme huyu samaki mmoja naenda kumkopesha sijui kama nitalipwa,
Na huyu mwengine naenda kulipa deni sijui kama nitalimaliza na huyu wa tatu naenda kumtupa.

Mfalme akachukizwa kwa majibu yale akaamuru anyang'anywe wale samaki nae atupwe gerezani,Akiwa kwenye Kasri Mfalme akaamuru yule mvuvi aletwe mbele yake ili amuhoji.Kwanini umekataa kuniuzia mimi samaki wakati unaenda kumkopesha tena hujui kama utalipwa,,? Wapili unaenda kulipa deni na hujui kama utalimaliza,,? Kisha mwengine unaenda kumtupa wakati mimi nina shida na samaki,,?

Mvuvi akamjibu Mfalme
Huyu ninae kwenda kukopesha sijui kama nitalipwa naenda kuwapa wanangu
Kwani kuwaudumia watoto hujui kama na wao watakuhudumia.

Na huyu ni nae kwenda kulipa deni sijui kama nitalimaliza nawapelekea wazazi wangu,
Kwa waliyo nitendea siwezi kuwalipa hata niwape nini.

Na huyu ninae kwenda kumtupa naenda kumpa Mkewangu,Kwani hao hawajui kushukuru wala kutosheka, hata uwape nini siku akicharuka tu atasema hujamfanyia chochote tokea umuoe.