MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO ' FASIHI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO ' FASIHI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' FASIHI'

Neno *fasihi* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. *Taaluma* inayohusu tungo za kisanaa za simulizi na andishi kwa mfano hadithi, ngano, methali, misemo, nahau, mashairi, tenzi, riwaya na tamthilia; Fasihi andishi; kazi ya fasihi kwa mfano riwaya na tamthilia katika maandishi; taaluma inayohusu tungo zinazodhihirisha sanaa ya lugha.

2. *(Kivumishi)* : -enye lugha safi na nzuri;
-enye usahihi wa kutamkwa, - enye usafi wa maneno, na usahihi wa maana na matumizi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *fasihi* ( soma: *faswiihun/faswiihan/,faswiihin* *فصيح* ) lina maana zifuatazo:

1. *Kivumishi* : mtu mwenye uwezo wa kuweka wazi tungo za lugha na anayeteua maneno yafaayo kisarufi, kimaana na kijamii na kuyaepuka yaliyo kinyume chake.

2. *Kivumishi* : Maneno fasihi ni maneno yaliyo wazi, na yenye kumvutia msikilizaji na yenye kukubalika akilini.

3. *Kivumishi* : Ulimi fasihi ni ule unaomsaidia mtu kutongoa tungo nzuri na zenye kuvutia.

4. *Nomino*: Maziwa safi yaliyosalia baada ya kuchujwa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *faswiihun* *فصيح*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *fasihi* lilichukua kutoka Kiarabu maana Kivumishi (-enye lugha safi na nzuri;  -enye usahihi wa kutamkwa, - enye usafi wa maneno, na usahihi wa maana na matumizi.) na likapewa maana mpya ya *taaluma inayohusu tungo zinazodhihirisha sanaa ya lugha,* taaluma ambayo katika lugha ya Kiarabu inajulikana kwa jina la *ADABU/AADAABU (* Soma: *Aadaabun/Aadaaban/Aadaab آداب* (Taaluma inayohusika na zao bora la fikra lililo katika ushairi au nathari.)

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*