MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA MANENO 'HALISI' NA 'UHALIS'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA MANENO 'HALISI' NA 'UHALIS'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'HALISI' NA 'UHALISI'

Neno *halisi* katika lugha ya Kiswahili ni kitenzi elekezi chenye maana zifuatazo:

1. Halisi.a, endana, lingana na (bei).

2. Faa.

Neno hili *visawe* vyake ni maneno *stahiki*, *pendeza* , *shimiri* na *stahili* .
Neno hili linanyambulika na kupatikana neno *halisia* .

3. Neno hili ni Kihisishi chenye maana ya: *kisicho doa wala dosari; kilicho asilia.*

4. Neno hili pia ni kivumishi chenye maana ya:
(i) -enyewe ; *rafiki halisi* , rafiki hasa.
(ii) - a kweli bila ya uwiano au kufanana na -ingine.

5. Neno hili ni kielezi kwa maana ya: *pasipo mashaka,* *hasa* .

Neno *uhalisia* ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Hali ya kuwa bayana, halisi na sahihi.

2. Uhalali asilia wa kisheria.

3. Hali ya jambo, kitu au tendo lilivyo.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *halisi* ( soma: *khaaliswun/khaaliswan/khaaliswini* *خالص* ) lina maana zifuatazo:

1. Kilicho halali.

2. Kilicho safi; kisicho doa.

3. Rangi nyeupe iliyotakata; rangi nyeupe isiyo doa.

4. Kinachomhusu mtu maalumu.

5. Bidhaa isiyodaiwa kodi.

6. Rafiki/mwandani wa kweli.

Neno *uhalisi* si neno la Kiarabu bali limesanifiwa kutokana na neno la Kiarabu *halisi* *خالص* .

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *khaaliswun* *خالص*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *halisi* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika bali Kiswahili kikaongeza maana zingine.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*