MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'SAKAFU'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'SAKAFU'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' SAKAFU'

Neno *Sakafu* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Eneo la chini aghalabu ndani ya nyumba lililosakafiwa./eneo la chini aghalabu katika nyumba lakini hata nje ya nyumba ambalo hujengwa kwa mawe na mchanga    uliochanganywa na saruji  na kisha hutandazwa rojorojo ya saruji.

2. Sakafu moja au zaidi inayojengwa juu baada ya dari ya kwanza ya jengo la ghorofa; horofa.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *sakafu* ( **saqfun/saqfan/saqfin* *سقف* ) lina maana zifuatazo:

1. Paa la nyumba na mfano wake lililo juu mkabala na ardhi ya sehemu husika.

2. Mbingu/ kitu chochote kilicho juu chenye kufunika.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *sakafu*/ *saqf* *سقف*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili lilichukua maana ya neno ' *dari* ' katika lugha ya Kiarabu wakati neno ' *dari* ' likichukua maana ya neno ' *sakafu* '.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*