MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO ' DARI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO ' DARI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' DARI'.

Neno *Dari* (wingi: *Madari* ) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Sakafu ya juu ya nyumba iliyo baina ya paa na kuta za nyumba.

2. Sitaha/Staha; sehemu ya mbele au nyuma ya chombo kama Jahazi au mtumbwi iliyo na ubao wa kukalia au kuwekea vitu.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *dari* ( **daarun/daaran/daarin* *دار* ) lina maana zifuatazo:

1. Riziki.

2. (Kivumishi) -enye kuendelea mfululizo bila ya kukatika/kukoma.

3. Mahali panapoungana jengo na uga.

4. Nyumba  wanayoishi watu .

5. Mji/Nchi.

6. Kabila.

7. (Neno hili likianza na kiambishi 'al' likawa 'Al-Daar' (soma: Ad-Daar): mji wa Baghdad katika nchi ya Iraq.

8. (Likiongezwa neno 'Al-Salaam' (soma: As-Salaam) likawa 'Daaru Al-Salaam' (soma: Daarus Salaam): Pepo.

9. Likiongezwa neno 'Al-Qaraar' kikawa 'Daaru Al-Qaraar' (soma: Daaril Qaraar': Akhera/Ahera, kuzimu.

10. Likiongezwa neno 'Al-Harb' kikawa 'Daaru Al-Harbi' (soma: Daarul Harbi': miji ya maadui.

Katika Lugha ya Kiarabu neno sakafu ( *saqfun/saqfan/saqfin* *سقف*) ndio linalobeba maana ya neno 'dari' katika Kiswahili, 'sakafu ya juu ya nyumba iliyo baina ya paa na kuta za nyumba'.

Hii inaonesha kuwa neno hili ( *dari* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili  maana yake katika  lugha yake ya asili (Kiarabu) ilibadilika na kuchukua maana mpya zilizobainishwa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*