MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - USHAMIRISHAJI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: USHAMIRISHAJI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Makala hii itaangazia kwa kifupi maana ya ushamilishaji kwa mujibu wa wataalamu wanavyojaribu kuielezea, tutaangalia maana ya uelekezi kwa mujibu wa wataalamu ambao ndio hutupa mwelekeo wa uelewa  zaidi dhana nzima na sifa pamoja na viashiria vya ushamirishaji, pia tutaeleza aina za ushamirishaji pamoja na makundi ya ushamilishaji.
Kwa kuanza na maana ya ushamilishaji wataalamu wameifasili kama ifuatavyo;
grammar.about.com/old/dg/complent. Wanaeleza ushamilishaji ni hali ya kishazi tegemezi kusaidia kueleza au kufafanua maana kamili ya nomino au kitenzi katika sentensi. Fasili hii imejikita kuonesha ushamirishaji wa nomino na kitenzi bila kuangalia au kueleza ushamilishaji wa vivumishi, vihusishi na vitenzi kwa hata vivumishi vinaweza kutosheleza na kishazi tegemezi.
O’grady na wenzake (1996) wanaeleza ushamilishaji kwa kutoa maneno ambayo yanaweza kufanyiwa ushamilishaji kama vile nomino, kivumishi, kitenzi, kihusishi ambayo yanaweza kutoshelezwa na vishazi tegemezi. Mapungufu ya hoja hii ni kwamba hawajaonesha ushamirishaji wa kielezi lakini ukweli ni kwamba ni maneno yanaweza kufanyiwa ushamirishaji.
Hivyo tunaweza kusema ushamirishaji ni mchakato unaofanywa na vishazi tegemezi kutosheleza kitenzi, nomino kivumishi kielezi na kihusishi kinachotokea kwenye upande wa kiarifu au kutoa maelezo yaliyo ya lazima kukamilisha taarifa ya za kitenzi, nomino, kivumishi, kihusishi na kielezi.
Baada ya kufasili maana ya ushakilishaji sasa tunaweza kueleza kwa kifupi maana ya uelekezi. Wataalamu wameeleza maana ya uelekezi kama ifuatavyo;
Massamba (2004) anaeleza uelekezi kuwa ni kuwa ni hali ya uhusiano uliopo baina ya kitenzi na  vijenzi vingine vya muundo wa sentensi vinavyohusiana nacho. Kiini chake hasa ni kitenzi kuhitaji au kutohitaji yambwa. Hii ina maana kuwa anaposema kuwa kitenzi kuhitaji yambwa ana maana kuwa kitenzi kuambatana na kipashio kingine kilicho cha lazima.
                Mfano:  mwalimu anasoma kitabu
                             Juma anacheza mpira
Hivyo katika sentensi hizi vipashio vilivyo vya lazima ni kitabu na mpira.
Katika kutohitaji yambwa (si elekezi) ana maana kuwa kutoandamana na kipashio kingine au kutoandamana lakini hakuna ulazima.
                                Mfano: Rajabu amelala usingizi.
Hivyo neno “usingizi” si kipashi cha lazima katika sentensi hii.
Habwe na karanja (2004) wanasema kitenzi elekezi ni vitenzi vinavyoashilia vitendwa na hali ambayo huvuka mipaka na kuathiri maneno mengi ya sentensi. Maneno yanayoathiriwa huitwa yambwa tendwa au tendwa.
                  Mfano: jesse anampiga mama
                               Baba anakula machungwa.
Hivyo basi kitenzi “anampiga” kinauliza swali la nani na “anakula” swali “nini” hivyo vitenzi hivi ni elekezi ambapo vinaandamana na maneno yaliyo ya lazima kama vile “mama” na “machungwa”.
Pia vitenzi si elekezi, wanaelezea kuwa ni vitenzi ambavyo huwa havihitaji yambwa. Kwa maana kwamba vinajitoshereza katika matumizi yake.
                                 Mfano: jamesi amesinzia
                                             Asha anakimbia
Hivyo vitenzi (amesinzia) na (anakimbia) si elekezi kwa maana havihitaji yambwa. Hivyo basi uelekezi tunaewza kusema ni mchakato wa kitenzi kuchukua au kubeba au kutoandamana na yambwa.
Baada ya kufasili au kueleza maana ya uelekezi tuangalie tuangalie sifa za ushamirishaji: sifa hizo ni kama zifuatazo.
Kishazi tegemezi bebwa, huwa kinafanya kazi ya kuarifu pia kufanya kazi ya kutosheleza kitenzi, nomino, kitenzi na kihusishi. Ni lazima kitokee baada ya maneno haya kwa lengo la kujibu maswali ya kwa nini na nani kama yale yanayotokea kwenye uelekezi.
Hivyo baada ya kuangalia sifa hizi za usharishaji tuangalie viashiria vya ushamiklishaji:
Black (1998) na O’glady na wenzake (1996) wanatueleza kuwa viashiria vya ushamirishaji ni kama vile ya, kuwa, kwamba,kappa, kama lakini kuna kiashiria kingine kama vile (ku). Blacka (1998) amezungumzia suala la ushamirishaji wa vitenzi peke yake hajatuelezea wa vitenzi, nomino,vivumishi, vihusishi na vivumishi kama O’glady na wenzake.
Baaba ya kuangalia viashiria vya ushamirishaji tuangalie ushamirishaji unaweza kujidhihirisha katika vitenzi, nomino, vivumishi, vihusishi na vielezi. Hivyo tukianza na :
Ushamirishaji wa vitenzi, ni ushamirishaji unaotokana na vitenzi vinapohitaji kutoshelezwa si kwa nomino za kawaida bali kishazi tegemezi ambacho lazima kitokee kwa lengo la kitenzi husika kukamilisha taarifa/ utoa taarifa zinazojitosheleza
                      Mfano:   Baba alimwambia [asha] kuwa mama hatarudi nyumbani.
                                     Mwalimu alihuzunika kuwa wanafunzi walifeli somo lake.
Kishazi tegemezi kilichotokea baada ya yambwa “Asha” na kitenzi “alihuzunika” vinafanya kazi ya kutosheleza vitenzi / kukamilisha taarifa ya kitenzi.
Ushamirishaji wa vitenzi umegawanyika katika makundi manne ambayo ni kama ifuatavyo:
Vitenzi vya kusema, ni vile vitenzi ambavyo huwa vinatoa ripoti, matangazo, kuarifu jambo, kuambia au kueleza jambo au tukio fulani.
               Mfano:  Rais aliwatangazia wananchi kuwa atavunja baraza la mawaziri.
                             Komba alituambia kwamba wanafunzi wanaojituma kusoma watafaulu.
Katika sentensi hizi kishazi au vishazi vinavyotokea baada ya kitenzi “aliwatangazia” na “alituambia” vinafanya kazi ya kushamirisha vitenzi hivi au kukamilisha taarifa ya vitenzi.
Vitenzi vya kudadisi au kutaka kujua, ni vile vitenzi ambavyo huwa vinafanya kazi ya uchanganuzi, kuuliza na kufanya upelelezi kuhusu kitu fulani au jambo.
                         Mfano: Juma alitaka kujua kwamba nani anafuja mali za umma
                Asha alichunguzakuwa wanafunzi wengi wanaishi kwa kutegemea fedha yamkopo.
Vishazi tegemezi vilivyopigiwa msitari vinafanya kazi ya ushamirishaji wa vitenzi  “alitaka” na “alichunguza”.
Vitenzi vya kutendesha, hivi ni vitenzi vya kuamuru, kuagiza, kuruhusu, kulazimisha, au omba kufanyika kwa jambo fulani.
                    Mfano:  Wazazi aliwasihi watoto kusoma kwa bidii ili wafaulu mitihani yao.
                                  Rais aliamuru kwamba wanajeshi walinde mipaka ya nchi.
Hivyo vishazi hivi vinafanya kazi ya kushamirisha “waliwashawishi” na “aliamulu” ambapo vinafanya kazi ya kutoshereza vitenzi.
Vitenzi vya kuhisina kuamua, hivi ni vitenzi vya pande, furahi, kataa, jaribu, thubutu, fikiria na kusudia
                   Mfano:  Wanafunzi walikataa kuwa hawawezi acha kudai haki zao.
                                 Mama alimkataza Juma kuwa asichezee karibu na kisima.
Vishazi hivyo vinafanya ya kutosheleza “walikataa” na “alimkataa”.
Ushamirishaji wa nomino, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kuelezea au kufafanua au kutosheleza  nomino ambayo inakuwa hijakamilika inayotokea katika sehemu ya kirifu.
                                   Mfano: ameacha maagizo kwamba mwanae amfuate.
 Kishazi tegemezi kilichotokea baada ya nomino “maagizo” kinafanya kazi ya kutosheleza namino “maagizo”
Ushamilishaji wa nomino unafanana na ushamilishaji wa vitenzi vya kusema, kudadisi na kutendesha. Hivyo tunaweza kugawa nomino katika makundi matatu. Makundi hayo nia kama vile:
Nomino za kutendesha, ni nomino ambazo huwa ambazo huwa zinaonesha hali ya kuamuru, kuruhusu, kuagiza kutaka, kulazimisha na kuomba.
               Mfano: Imetolewa amri kwamba wamanchi wasichechee migomo ya vyimbo vya dola.
                            Ametoa maagizo kuwa wanafunzi wote tuondoke kesho hapa chuoni.
Vishazi vilivyotokea baada ya nomino “amri”na” maagizo” vinafanya kazi ya kutosheleza nomino hizi.
Nomino za kudadisi au kutaka kujua, ni nomino ambazo huwa ziafanya kazi ya kuchunguza, kuuliza au kuliza jambo fulani.
                              Mfano:    sina uhakika kama maelezo aliyatoa ni ya kweli
                                             Sina mashaka  kama maelezo yake si sahihi.
                                             Sina uhakika kama uufafanuzi wako unajitosheleza.
Vishazi vinavyotokea baada ya nomino vinafanya kazi ya kutosheleza nomino “uhakika” na “mashaka”.
Nimino za kusema, ni nomino zinazotoa ripoti, tangaza, arifu, ambia, na eleza jambo au tukio fulani.
                         Mfano: Ametoa matangazo kwamba watu wote wafike kwenye mkutano.
                                      Tumetoa taarifa kwamba wanawake wengi ni wavivu.
Vishazi vinavyotokea baada ya nomino vinafanya kazi ya kushamirisha nomino husika au kutosheleza nomino hii.
Ushamilishaji wa vivumishi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kivumishi kinachotokea kwenye kiarifu. Ushamilishaji huu hufanana na ushamilishaji wa vitenzi vya kuhisi au kuamuru.
                                Mfano: haikuwa rahisi kumuua Simba kwa mishale.
                             Ni vigumu kumwamini msichana ambaye humfahamu historia yake ya maisha.
Hivyo vishazi vinavyotokea baada ya kivumishi “rahisi” na “vigumu” inatumika kutosheleza vivumishi hivi ambavyo havikamilishi maana ya tungo.
Ushamirishaji wa vihusishi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kihusishi kinachotokea upande wa kiarifu ambacho huwa ni lazima kitokee baada ya kihusishi.
               Mfano:  Juma alifaulu kwa kusoma kwa bidii
                           Mwalimu alituambia ya kwamba tusipokuwa makini tutafeli vibayamitihani.
                           Neno la Mungu linasema ya kuwa kumcha bwana ni chanzo chamaarifa.
Hivyo vishazi hivo vinafanya kazi ya kazi ya kutosheleza kihusishi.
Ushamilishaji wa vielezi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kielezi kinachotokea upande wa kiarifu ambacho huwa na lazima kutokea baada ya kihusishi.
                  Mfano: John anatembea polepole kama mgonjwa anyeumwa miguu.
                               Asha anakula harakaharaka kama mtu ambaye hajawahi kula siku kumi.
Hivyo vishazi vinafanya kazi ya kutosheleza kielezi.
Hivyo basi ushamirishaji katika Kiswahili unasaidia kuondoa maswali ya nini? Na nani?. Hivyo ushamirishaji unafanya kazi ya kutoa taarifa zilizo kamilika.
MAREJEO
Black, C.A (1998) A step by Introduction to The Government and Biding Theory of Syntax. SIL-
                   Mexico Branch and Univerisity of North Dakota.
grammar.about.com/od/c/g/complement.
Habwe, J na Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix.
Massamba, D.P.B (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.