MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - USAYANSI WA ISIMU

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: USAYANSI WA ISIMU
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Wanaisimu waliochunguza lugha waliyumbishwa na mitazamo na mielekeo yao ndipo wakaona haja ya kuichunguza kisayansi.
           SIFA ZA UCHAMBUZI WA LUGHA KISAYANSI
(1) Uwazi
Hii inawataka wanaisimu kuweka hoja zao wazi bila hofu yoyote ile. Hii ina maana ya kwamba mada ya uchunguzi yafaa kuelezwa kwa undani kabisa. Yote ambayo wanaisimu watayasema kuhusu mada yawe kwa uwazi na kwa njia ya kueleweka kwa urahisi. Kwa mfano mawanda aliyoyatumia katika kazi yake yawe na uwazi na ukamilifu ambao unafaa kuzingatiwa katika uwekaji wa maneno, utengaji wa hoja na hata uchunguzi wa data.
(2) Upangilifu na utaratibu maalum 
Hoja zote zinapaswa kupangwa vizuri katika
taaluma zote za kisayansi, kwa utaratibu  maalum mambo yote hufuatwa hatua kwa hatua. Wanaisimu
hufuata utaratibu katika kuchambua kazi yake ifaavyo.Mwanaisimu hatakiwi kufanya
kazi yake kiholela holela.
(3) Uchechefu
Hapa ni pale wanaismu wanapofaulu
kueleza tofauti zote zilizomo katika kongoo linalochunguzwa  hatimaye katika
lugha hiyo yote.
(4) Wanaisimu kuweza kuifafanua kazi yao jinsi inavyotakikana
Hii ni hatua ambapo mwanaisimu
anapofanikiwa kuifafanua kazi yake kwa undani kabisa, katika viwango
vyote.Viwango hivi ni kama vile vya kifonolojia, mfumo wa sauti na kimofolojia.
(5) Mwana isimu anafaa kuichunguza kazi yake kwa kina kabisa
 
Mwanaisimu anapofanikiwa kueleza yale yote ambayo
ametafiti kwa kina, bila kuacha au kupuuza kitu chochote anachochunguza.