MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - KIDATO CHA PILI: UTATA KATIKA MAWASILIANO

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: KIDATO CHA PILI: UTATA KATIKA MAWASILIANO
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Utata katika Mawasiliano
Utata ni hali ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hiyo tungo tata ni tungo ambayo inaweza kuwa na maana zaidi ya moja.


Sababu za Utata
Elezea Sababu za Utata

Utata katika tungo hutokea kwa sababu zifuatazo:
  1. Neno kuwa na maana zaidi ya moja, kwa mfano neno mbuzi, kata n.k.
  2. Kutozingatia taratibu za uandishi, Mfano; Tulimkuta Nyammy na rafiki yake, Mazala vs Tulimkuta Nyammy na rafiki yake Mazala. Katika sentensi hizi alama (,) ndio huleta tofauti, sentensi ya kwanza inamaana kulikuwa na watu wawili Nyammy na rafiki yake aitwaye Mazala na sentensi ya pili isiyo na alama (,) inamaanisha kulikuwa na watu wawili Nyammy na mtu mwingine ambaye ni rafiki yake Mazala
  3. Kutumia maneno bila kuzingatia muktadha wa matumizi ya maneno hayo.
  4. Utamkaji wa maneno. Wakati mwingine utata unaweza kujitokeza katika matamshi tu, ili hali katika maandishi utata hauonekani. Kwa mfano; Mimina wewe, katika maandishi linaweza kuandikwa mimi na wewe, na hivyo kuondoa utata.
  5. Mjengo wa maneno. Utata huu huzuka katika vitenzi kama pigia. Chanzo cha utata katika kitenzi hiki ni kiambishi –i-. Kiambishi hiki kinaweza kumaanisha: kwa ajili ya…, kwa sababu ya.., kwa kutumia chombo fulani.., au mahali fulani.

Mfano:
  • Alimpigia ukorofi wake (kwa sababu ya)
  • Alimpigia kiatu (kifaa)
  • Alimpigia ndani (mahali)

Mifano ya utata katika tungo
  1. Patience amemwandikia Lilian barua:Sentensi hii huweza kuwa na maana kuwa Patience ameandika barua kwenda kwa Lilian au Patience ameandika barua kwa niaba ya Lilian
  2. Umefanikiwa kununua mbuzi?Sentensi hii huweza kumaanisha ununuzi wa mbuzi mnyama au mbuzi kifaa cha kukunia nazi.
  3. Alimkuta amelala kwenye nyumba ya wageni:Sentensi hii huweza kumaanisha, nyumba ya mtu lakini inatumika kwa ajili ya wageni kwa malipo au ni nyumba inayomilikiwa na watu ambao ni wageni katika eneo lile.
  4. Attu ametumwa na Aritamba:Sentensi hii inaweza kueleweka kumaanisha, Aritamba amemtuma Attu au Attu na Aritamba wametumwa wote kwa pamoja.
  ZOEZI  
Zifuatazo ni sababu za utata, isipokuwa:

A
Kutumia maneno ya picha

B
Neno kuwa na maana zaidi ya moja

C
kutumia maneno bila kuzingatia muktadha husika

D
Umahiri wa lugha

Neno ‘mbuzi’ ni tata, kwa sababu___

A
Lina maana moja tu

B
Lina maana zaidi ya moja

C
Lina maana iliyofichika

D
Ni neno la Kiswahili

Utata unaojitokeza katika mazungumzo pekee husababishwa na nini?

A
Mjengo wa maneno

B
Maana zaidi ya moja katika neno

C
Utamkaji wa maneno

D
Kutozingatia taratibu za uandishi

Utata katika matumizi ya vitenzi kama vile ‘pigia’ husababishwa na___

A
Neno kuwa na maana zaidi ya moja

B
Utamkaji wa neno

C
Kutozingatia taratibu za uandishi

D
Mjengo wa neno

“Juma ametumwa na Rama” Utata wa tungo hii ni wa kutozingatia nini?

A
Matumizi ya picha

B
Utamkaji wa maneno

C
Utumiaji wa neno wa katika muktadha wake

D
Taratibu za uandishi