MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA TANO: DHANNA YA MZIZI NA SHINA

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA TANO: DHANNA YA MZIZI NA SHINA
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MUHADHARA WA TANO: DHANNA YA MZIZI NA SHINA
MAANA YA MZIZI
Mzizi/kiini cha neno ni ile sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolewa viambishi awali na tamati.
Au
Mzizi ni sehemu ya neno isiyobadilika baada ya neno kufanyiwa mnyambuliko.
Mzizi huweza kujitokeza katika aina mbalimbali za maneno kama vile vitenzi, nomino, vivumishi, viwakilishi, n.k
(i) Mzizi katika vitenzi
Mfano:
– Juma anasoma kitabu
– Baba analima shamba
ii) Mzizi katika nomino
mfano:
– kusoma kwake tunakupenda
– mtoto anacheza
– watoto wanacheza
– kijana  analima
– vijana  wanalima
iii) Mzizi katika vivumishi
Mfano
– mwema-wema
– bovu-mabovu
– mdogo-wadogo
iv) Mzizi katika viwakilishi
mfano
– Ambaye anaumwa aje
– Ambalo umenunua halifai
– Ambacho umesema kinakera
– mimi-miye
– sisi-siye
– wewe-weye
– nyinyi-nyiye
DHIMA YA MZIZI
Mzizi hutumika kuunda maneno mapya kwa kutumia viambishi.
Mfano
  1. - Lima-limia-kilimo-mkulima- Mzizi husaidia kutambua mofolojia ya neno- Mzizi husaidia kupanua taarifa za neno kwa kupachika viambishi mbalimbali- Mzizi husaidia kuleta  upatanisho wa kisanifu baina ya neno na maneno mengine.
JINSI YA KUTAMBUA MZIZI
Utambuzi wa mzizi katika neno huweza kufanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile:
1. Njia ya mnyambuliko
Ili kupata mzizi wa neno kwa njia hii sharti neno linyambuliwe kwanza. Neno likishanyambuliwa sehemu isiyobadilika huwa ndiyo mzizi.
Mfano
Soma
Somesha
Somewa
Tulimsomesha
Msomi
2. Mbinu ya  umoja na wingi
Njia hii hufaa zaidi kwa maneno yenye asili ya nomino, vivumishi na viwakilishi
Mfano
Umoja   wingi
Mtoto    watoto
θJembe   majembe
Kijana vijana
Mdogo wadogo

3. Njia ya umbo la ndani

Hapa neno hupaswa kurudishwa katika umbo lake la ndani.
Kama ni kitenzi kikiishia na irabu “a” basi hiyo irabu “a” ikiondolewa kinachobaki ndiyo mzizi.
Iwapo kitenzi kina asili ya kigeni kitaishia na irabu tofauti na “a” na hilo neno zima huweza kuwa ndio mzizi/shina.
Mfano
Neno                              Muundo ndani         Mzizi
Walisomeshwa                        soma             -som-
Walipikishwa                             pika             -pik-
Tutamsalia                               Sali             -Sali-
Mnastarehesha                           starehe           starehe
Shukuru 
                                shukuru           shukur-
MAANA YA SHINA
Shina la neno ni mzizi wowote wa neno uliofungiliwa kiambishi tamati maana.
Mfano
Mzizi   Shina
Pig+a  – piga
Som+a  – soma
imb+a  — imba
SHINA = MZIZI+a
MZIZI = SHINA-a
 
Uhusiano wa mzizi na mofimu nyingine katika maneno
Mzizi huwa na viambishi ambavyo hupachikwa mwanzoni na /au mwishoni mwa mzizi wa neno.
[Image: SAM_1505.JPG]
===> Viambishi awali    V.A) hufanya kazi kama vile kudokeza nafsi, njeo, urejeshi, yambwa, yambiwa n.k
===> Viambishi tamati (V.T) hufanya kazi ya kudokeza kauli mbalimbali za matendo.