MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - NYAKATI ZA KISWAHILI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: NYAKATI ZA KISWAHILI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Nyakati za Kiswahili
Nyakati katika lugha hutuonesha kitendo chafanyika lini.
Mifano ya Nyakati
  • Wakati Uliopita – LI
  • Wakati Timilifu (uliopita muda mfupi) – ME
  • Wakati Uliopo – NA
  • Wakati Ujao – TA
  • Wakati wa Mazoea – HU
  • Wakati Usiodhihirika – A
  • Wakati Timilifu Usiodhihirika – KA
Wakati Uliopita – LI
Wakati huu hurejelea kitendo kilichofanyika muda mrefu uliopita. Vitenzi katika wakati uliopita hutumia kiambishi “LI”
kwa mfano : a-li-sema, ni-li-fika, wa-li-timuliwa
  • Mwanafunzi alifukuzwa shuleni.
  • Mzee Katili alimpiga Bi Kazi.
Wakati Timilifu – Uliopita Muda Mfupi – ME
Wakati timilifu huonyesha kitendo ambacho kimekamilika sasa hivi au muda usio mrefu. Hutumia kiambishi ME katika vitenzi.
kwa mfano: nimeshiba, limeanguka, kimeharibika
  • Mkoba wa babu umepasuka.
  • Jicho la Bi Kijicho limetoboka
  • Mzee Mauti ameaga dunia.
Wakati Uliopo – NA
Wakati uliopo huonyesha kitendo kinachoendela kufanyika sasa hivi. Hutumia kiambishi “NA” katika vitenzi.
kwa mfano: a-na-soma, tu-na-kueleza, zi-na-angamia
  • Nyanya anasimulia hadithi
  • Mtoto wa jirani anapigwa na mama yake
  • Mvua inanyesha kwa ujeuri.
Wakati Ujao – TA
Huchukua kiambishi “TA” na hurejelea kitendo ambacho bado hakijafanyika lakini kinatarajiwa kufanyika..
kwa mfano: atakupa, kitajulikana, utapokelewa
  • Mtoto atalifunga dirisha litakalokuwa likiingiza hewa.
  • Je, utaenda sokoni kesho kutwa?
Wakati wa Mazoea – HU
Hutumia kiambishi “HU” na hurejelea kitendo ambacho hufanyika mara kwa mara au kila siku n.k.
kwa mfano: hutembea, husoma, huzilinda
  • Dkt. Matumbo hutibu wagonjwa.
  • Mchungwa ule huzaa machungwa matamu.
Wakati Usiodhihirika – A
Hutumia kiambishi cha ngeli au nafsi pamoja na kiungo “A” kurejelea kitendo kinachoendelea kutendeka katika wakati usiodhihirika.
kwa mfano: achukua, zapepea, twaangamia
  • Baba atusubiri nyumbani.
  • Vitabu vyako vyote vyachomeka
Wakati Timilifu Usiodhihirika – KA
Hutumia kiungo “KA” kurejelea kitendo ambacho kinakamilika katika wakati usiojulika. Pia hutumika kurejelea kitendo kifanyika baada ya kingine. Hutumiwa katika masimulizi.
kwa mfano: ikawalemea, tukazichukua, likampendeza
  • Latifa akaangalia juu akamwona nyoka.
  • Akawanyeshea mana wakiwa jangwani