MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MAUMBO YA NOMINO ZA KIMAKUNDUCHI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MAUMBO YA NOMINO ZA KIMAKUNDUCHI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MAUMBO YA NOMINO ZA KIMAKUNDUCHI
Katika kuzichunguza nomino za Kimakunduchi imebainika kuwa ni nyingi zao ni nomino za kawaida ambazo hazitofautiani mno na nomino za lugha sanifu. Tofauti iliyoonekana kwamba kwa baadhi ya wakati, nomino za Kimakunduchi huwemo katika maumbo ya kilahaja; na hivyo kuyafanya makundi ya geli za majina kubadilika baadhi yao kwa mujibu wa kigezo cha upatanishi wa kisarufi. Tuchunguze mifano ifuatayo:
Kundi A
Mwana kagu (Mtoto ameanguka)
Wana wagu (Watoto wameanguka)
Kundi B
Mjiti ukatiki (Mti umekatika)
Mijiti ikatiki (Miti imekatika)
Kundi C
Dicho liumii (Jicho limeumia)
Macho yaumii (Macho yameumia)
Kundi D
Cheti chake chaga (Cheti chake kimepotea)
Vyeti vyake vyaga (Vyeti vyake vimepotea)
Kundi E
Uvivu umgwishi (Uvivu umemwangusha)
Wivu umwachisi (Wivu umemwachisha)
Kundi F
Konde yake ilimwa (Konde yake imelimwa)
Konde zake zilimwa (Konde zake zimelimwa)
Kundi G
Ugonjwa wake umtuu kitako (Ugonjwa wake umemweka kitako)
Kundi H
Kwimba kwake kunachekesha (Kuimba kwake kunachekesha)
Kwiba kunasikitisha (Kuiba kunasikitisha)
Kundi I
Mahaa vake vanafurahisha (Mahali pake panafurahisha)
Vyumbani mwake mnanukia (Vyumbani mwake mnanukia)
Kundi J
Maji yamemwagiki (Maji yamemwagika)
Kundi K
Chuvi isi (Chumvi imekwisha)
Tunapoichunguza vyema mifano iliyomo kwenye makundi hayo, tutabaini kuwa kila kundi linaweza kuunda ‘kundi la ngeli’ fulani. Kwa mfano, Kundi A linazaa ‘KAWA’ badala ya ‘YU/A-WA’, Kundi B kwa ‘U-I’, Kundi C kwa ‘LI-YA’, Kundi D kwa ‘CHA-VYA’ badala ya ‘KI-VI’, Kundi E kwa ‘U’, Kundi F kwa ‘I-ZI’, Kundi G kwa ‘U-YA’, Kundi H kwa ‘KU’, Kundi I kwa ‘M, VA’ badala ya ‘PA MU KU’, Kundi J kwa ‘YA’ na Kundi K kwa ‘I’.
Mjengeko huo wa makundi ya ngeli uliyo kinyume kidogo na mgawanyiko wa makundi hayo katika lugha sanifu, huathiri watumizi wa lugha sanifu wa Makunduchi kwa kiasi kikubwa. Hii huwafanya wanafunzi hao wakati wanapotunga sentensi zao waziingize ulahaja zaidi kuliko usanifu unaotarajiwa. Mwanafunzi hutoa sentensi kama hii ‘ Mtoto kanakuja’ au ‘Watoto wanakuja’ badala ya ‘Mtoto yuaja/anakuja’ au ‘Watoto waja/wanakuja’.