MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - UBORA NA UDHAIFU WA NGELI ZA KISINTAKSIA/KISASA

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: UBORA NA UDHAIFU WA NGELI ZA KISINTAKSIA/KISASA
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
UBORA WA MTAZAMO WA KISASA
Kigezo cha kisintaksia kinachotumiwa katika mtazamo wa kisasa kugawa ngeli kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi kina ubora wake kama ifuatavyo:
  • Kimepunguza makundi mengi ya ngeli za nomino
  • Ni rahisi kuzikariri kwani ni chache.
  • Kila nomino huweza kuingia katika ngeli yake kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi.
  • Nomino hupangwa katika ngeli zake kulingana na sifa na hadhi yake.
  • Husaidia kubaini umoja na wingi wa nomino zisizo na maumbo dhahiri ya idadi.
  • Kigezo hiki kimepunguza kujirudiarudia kwa ngeli.
  • Husaidia kubainisha uhusiano wa nomino na maneno mengine katika tungo.
  • Husaidia kuonesha urejeshi wa vitenzi na nomino zake.
UDHAIFU WA MTAZAMO WA KISASA
  • Bado kuna ngeli za nomino zinazojirudia mf. Ngeli ya 2,6 na 7 umoja zinatumia u.
  • Ngeli ya kwanza umoja ina viambishi viwili (Yu/A)
  • Bado kuna nomino zenye kuleta mgogoro katika ngeli mf. Makala, Jambazi, marashi.
  • Pamoja na umoja na wingi kutawala, kigezo cha sifa ya nomino hujitokeza ili kuepuka kuchanganya majina yenye sifa na hadhi tofauti mf. Kinyonga hukubali zaidi ngeli ya (KI-VI) lakini huwekwa katika ngeli ya kwanza kwa sifa ya kiumbe hai.
  • Kigezo hiki hakijaweza kuonesha mofolojia ya nomino.