MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MFANO WA KISASILI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MFANO WA KISASILI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
KISASILI
Kisasili ni hadithi fupi zinazoelezea asili ya jambo au maumbile fulani. Wahusika wake huwa ni wadudu, wanyama, binadamu, miungu na vitu visivyo na uhai, lakini huwa na hadhi ya kibinadamu. Mara nyingi kisasili huanza na “paukwa!”  mfano ni Kisa cha Nguruwe kukosa mkia. 
Paukwa! (Aliuliza bibi)
Pakawa! (Waliitikia wajukuu zake)
Hapo zamani za kale, palitokea ubishi kati ya nguruwe na ng’ombe. Kila mmoja akawa anatamba kuwa ana nguvu kuliko mwenzake. Bahati nzuri akatokea sungura akawauliza, “Kulikoni mbona mnabishana hivyo?” Nguruwe na ng’ombe wakamweleza chanzo cha ubishi wao.
Nguruwe akaanza kumkashifu mwenzake ng’ombe, “Huyu hanijui mimi! Ananisikia tu, nitamvunjavunja mbavu asahau hata njia ya kurudi kwao” Ng’ombe naye akadakia, “Wewe ni bwana mdogo tu, huo ufupi na unene wako hauwezi kunibabaisha.”
Sungura akasikiliza halafu akasema, “Hakuna sababu ya kubishana, mimi naona mshindane.” Wote wakakubali. Sungura akasema, “Nitawafunga mikia yenu pamoja. Nikihesabu moja, mbili, tatu muanze kuvutana. Yule ambaye mkia wake utakatika atakuwa ameshindwa.”
Basi wajukuu zangu, wote wakasema sawa. Nguruwe akamtahadharisha ng’ombe, “Mkia wako utakuwa halali yangu” Ng’ombe akaingiwa na woga, akatulia tuli kama maji mtungini, lakini akaamua kujikaza kisabuni.
Basi sungura baada ya kuwafunga mikia akahesabu moja, mbili, tatu wakaanza kuvutana. Wajukuu zangu mngekuwepo mngejionea kivumbi na jasho. Si mnajua wajukuu zangu, wapiganapo fahari wawili? Akauliza bibi. “Ziumiazo nyasi,” wakajibu wajukuu zake.
Punde si punde zilisikika kelele Guuuuu! Guuuuu! Guuuuu! na kishindo kikubwa puuu uu! Lahaula! Mkia wa nguruwe ulikatika, akaanguka chini puuuu na pua ikabonyea. Nguruwe akalia kwa uchungu, damu ikamtoka kwa wingi kama bomba la maji. Ng’ombe alikuwa mshindi.
Sungura kuona vile akakichukua kipande cha mkia; huyoooo! Akampelekea rafiki yake fisi. Nguruwe akajuta sana kwa nini alikubali ushindani.
Basi wajukuu zangu, hadi leo nguruwe na ukoo wake hawana mikia na pia pua zao zimebonyea. Wajukuu zake wakacheka na kusema, “Kumbe! Ndiyo maana nguruwe wana mikia mifupi”