MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - KISASILI CHA JOGOO – KWANINI JOGOO HUWIKA?

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: KISASILI CHA JOGOO – KWANINI JOGOO HUWIKA?
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Paukwa!
Pakawa!
Hapo zamani za zamani, siku moja palitokea mafuriko makubwa sana. Wanyama na ndege wote walipata taabu kubwa. Taratibu maji yalijaa nchini hata kufikia mahali ambapo jogoo alikuwa amesimama baada ya kuchoka mno. Jogoo alitweta na kuhangaika kabisa. Kwa bahati nzuri ndege wengine walioruka juu zaidi walimwona na kumwonea huruma. Hivyo wakakata shauri la kumsaidia.
Haraka sana ndege hao walikwenda juu ya mlima mrefu sana, wakaokota huko ufito na kuja nao mpaka alipokuwa jogoo. Wenyewe wakajigawa makundi mawili. Kundi moja likashika ncha moja ya ufito na jingine likashika upande wa pili. Kisha wakamwambia jogoo asimame katikati juu ya ufito, huku ameshikilia kwa nguvu. Kwa pamoja wakamwinua juu na kuruka naye hadi mlima mrefu mahali pasipoweza kufikiwa na mafuriko. Akawa ameokoka kabisa.
Jogoo alifurahishwa sana na kitendo hicho cha kumwokoa. Hata mafuriko yalipokwisha, jogoo aliwauliza ndege, “sasa rafiki zangu wapenzi, nilikuwa nimekufa, nanyi mmeniokoa. Je, nami niwafanyie nini mpate nanyi kufurahi?”
Ndege kwa pamoja wakamjibu, “Sisi hatutaki utulipe kitu. Ila sote tunapenda kuwahi kuamka. Lakini wakati mwingine tunachelewa. Kwa hiyo ukihiyari tunaomba uwe unatuamsha.” Jogoo akajibu, “Nimehiyari kabisa; nitajitahidi kuwaamsha mapema kila siku.”
Tangu hapo jogoo huwika kila siku: kokoikoo maana yake kumekucha, amkeni wapenzi; Ooo! yaani. Nilikufa, asanteni! Huwika asubuhi na mapema ili kuwaamsha wafadhili wake. Huwika na mchana ili kuzoeza sauti yake isikwame.