MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - KISA CHA MJANE NA MBWA WAKE

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: KISA CHA MJANE NA MBWA WAKE
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Hadithi hadithi!
Hadithi njoo!
Hapo zamani za zamani palikuwa na baba mjane na mbwa wake. Nao walipendana sana. Kwa siku nyingi walikaa katika kibanda chao kidogo mbali mwituni.
Ikaondokea siku moja katika zungukazunguka yake ya kutafuta chakula, baba mjane huyo aliokota kioo kizuri akakiweka kibandani mwake.
Mchana mmoja, wakati amepumzika kibandani mwao, mbwa akakiona kile kioo kimetundikwa ukutani. Kuchungulia zaidi akaona mbwa mwingine wa kimo chake na rangi yake amesimama mbele yake. Pale pale mbwa akaanza kubweka ili kumwogofya yule mbwa mgeni. Kumbe jinsi alivyobweka ndivyo na yule mbwa wa pili alivyoonekana kubweka pia. Asitake mshindani, mbwa alimrukia kwa makucha yule mbwa mgeni. Kumbe badala ya kumpiga mbwa mgeni makucha yalifikia ukutani. Makucha yakaumia. Hapo mbwa kwa hasira yote alitoa meno na kumrukia ili amwume. Lakini safari hii alikipiga kioo na kukivunja kabisa.
Baba mjane alipotahamaki alimwambia mbwa wake, “Unajisumbua, rafiki yangu. Mbona unagombana na kivuli chako, wala siyo mbwa!” Mbwa akaona haya sana.