MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - Majina ya ukoo/ familia katika lugha ya kiswahili

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: Majina ya ukoo/ familia katika lugha ya kiswahili
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Haya ni majina ya heshima yanayotumiwa na watu mbalimbali katika familia 
kulingana na uhusiano wao. Pia huitwa msamiati wa nasaba/jamaa/jamii
Familia Ndogo
Lengo letu ni kufundisha na kuendeleza lugha ya kiswahili kama kitambulisho cha jamii.
Hii ni familia ya karibu ambayo huhusisha tu wazazi na watoto wao. 
1. baba : ( father ) 
ni mzazi wa kiume. 
2. mama : ( mother ) 
mama ni mzazi wa kike. 
3. mwana : ( child ) 
mtoto wako 
4. mzazi : ( parent ) 
mtu aliyekuzaa 
5. ndugu : ( sibling ) 
mtoto wa mzazi/wazazi wako. Mara nyingi ’ndugu’ hutumika kurejelea watoto waliozaliwa baada yako, au watoto wa kiume waliozaliwa na wazazi wako. 
6. kaka : ( brother ) 
mvulana aliyezaliwa na mzazi/wazazi wako. Aghalabu kaka hurejelea mvulana aliyekutangulia kuzaliwa. 
7. dada : ( sister ) 
msichana aliyezaliwa na mzazi/wazazi wako. Aghalabu dada hutumika kurejelea wasichana waliokutangulia kuzaliwa. 
8. bin : ( son, mwana ) 
mtoto wa kiume
9. binti : ( daughter ) 
mtoto wa kike. 
10. kifungua mimba : ( first born ) 
mtoto wa kwanza kuzaliwa 
11. kitinda mimba : ( last born ) 
mtoto wa mwisho kuzaliwa 
12. mapacha : ( twins ) 
watoto wawili waliozaliwa siku moja na mama mmoja 
13. mke : ( bibi, wife ) 
mwanamke mliyefunga ndoa pamoja kuanzisha familia. 
14. mume : ( husband ) 
mwanamume mliyefunga ndoa pamoja ili kuanzisha familia. 
15. baba wa kambo  : ( stepfather ) 
mwanaume aliyeoa mamako, na ambaye si baba yako wa damu 
16. mama wa kambo : ( stepmother ) 
mwanamke aliyeolewa na babako, na ambaye si mama yako wa damu