MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: MKE NA MUME

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: MKE NA MUME
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MUME:?
Mke wangu umenuna, nambie tatizo nini
Toka juzi nakuona, umechukia rohoni
Pia nikaona jana, umejawa kisirani
Mumeo furaha sina, kwa sababu yako hani
MKE:?
Ni kweli nimechukia, tena moyo waniuma
Mume wangu naumia, mpaka napata homa
Mambo ulonifanyia, nishachoka ninasema
Kila siku kuumia, bora nirudi kwa mama
MUME:?
Mke wangu we funguka, nijue tatizo nini
bado wanipa mashaka, Huongei kwa yakini
Sema nini unataka, nikupatie mwandani
Nieleze kwa hakika, nasikiza kwa makini
MKE:?
Sana nimevumilia, ila sasa nimechoka
Mume ninakuambia, unipe yangu talaka
Kutwa kukufumania, mpaka kwenye vichaka
Umempanda rukia, ukimwi ushauteka
MUME:?
Lini wewe umeona, ya watu unasikia
Mambo hayo mimi sina, elewa nayokwambia
Mke nakupenda sana, wengine napuuzia
Maneno yaso namana, watu wamekuletea
MKE:?
Usijifanye wajua, mimi mwenyewe naona
Mwajuma nae asia, mara mbili kwenye kona
Ashura pia maria, hao wote nimeona
Majumbani mwaingia, mimi chonjo najibana
MUME:?
Mke wangu nisikie, haya ninayoyasema
Wale sio wangu mie, wale ni wa bosi juma
Na simu tumpigie, asikie akisema
Chaji moja niletee, simu yangu imezima
MKE:?
Mda chaji nimeleta, mpigie huyo juma
Usije leta utata, mengi sana sitosema
Kitu kitakachofata, kunijua utakoma
Mbona simu inaita, hapatikani wasema
MUME:?
Tatizo ni mtandao, nielewe mke wangu
Nenda hata kalete, kibao niweke miguu yangu
Unisikie mwenzio, nalonena mke wangu
Hebu we achana nao, tulizana mke wangu
MKE:?
Kichwani unanipanda, mume wangu nakuona
Hata kama nakupenda, ila kwa sasa hakuna
Roho yangu ishapinda, ulofanya unakana
Mbali nawe nitaenda, daima hutoniona
SULUHISHO?
MUME:?
Mke wangu ninakili, hayo yote ulosema
Usemayo ni ya kweli, nimelala na fatuma
Zaidi ya mala mbili, nikalala na rehema
Mke wangu tafadhali, kwako naja nalalama
MKE:?
We mwanaume malaya, Mimi bora niondoke.
Huso umejaa haya, Sitaki nihudhunike.
Umenitenda vibaya, Acha peka niteseke.
We mwanaume m,baya, Nipe changu niondoke.
MUME:?
Mke wangu ninatubu, napiga magoti kwako.
Nimelipata jawabu, sitaenda michepuko
Nimejifunza adabu, mi nakupenda mwenzako
Mke wangu mtabibu, nisamehe mume wako
MKE:?
Sawa nimekuelewa, hayo yote yameisha
Nataka kuheshimiwa, tuanze upya maisha
Usije kushaiwishiwa, thamani ukanishusha
Wewe ndiyo maridhawa, mume wangu wa maisha
M W I S H O
Mtunzi:Sefu Makanyila
Location:Jaribu Mpakani-KibitiĀ [Image: 1f1f9-1f1ff.svg]
Mawasiliano:+255787 141414