MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - KF 120: MASWALI YA VIKUNDI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: KF 120: MASWALI YA VIKUNDI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
[Image: maswali.png]
  1. “Vipengele vya kibunilizi na utumiaji wa wahusika katika kujadili dhamira kwenye kazi nyingi za  fasihi andishi ya kiswahili umekuwa ukibadilika toka enzi moja kwenda nyingine”. Muwe huru kutumia kazi zozote za kifasihi kithibitisha ukweli wa hoja hiyo.
  2. “Shaaban Robert katika Adili na Nduguze amefanikiwa kujenga dhamira zake kwa kutumia motifu ya safari”. Jadili.
  3. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya riwaya na mchango wa wajerumani kama koloni katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili kihistoria.
  4. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya tamthilia na mchango wa Wakenya katika kukua kwa tanzu hiyo.
  5. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya ushairi  na mchango wa wareno na waarabu katika kuenea kwa tanzu hiyo.
  6. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya ushairi na mchango wa wareno na waarabu katika kukua kwa tanzu hiyo.
  7. Bainisha kwa mifano mchango wa Shaaban Robert katika maendeleo ya fasihi andishi ya Kiswahili.
  8. Jadili jinsi Naratolojia katika Wasifu wa siti bint Saad unavyozipambanua dhamira kirahisi ndani ya riwaya hiyo .
  9. Utomeleaji katika diwani ya Kiswahili na Malenga unaonekana kuwa na faida na hasara katika kujadili dhamira kwenye diwani hiyo. Jadili.
  10.  Wahusika katika riwaya za kingano wanamchango gani katika kujadili dhamira za kazi ya fasihi kihistoria?
  11. Mgogoro wa mswahili ni nani unaathiri vipi maendeleo ya fasihi ya Kiswahili hususani kwenye upande wa dhamira?
  12. Eleza mchango wa wataalamu wafuatao katika kuibuka na kuendelea kwa riwaya ya Kiswahili:
  13. Edward Steere
  14. Carl Veltten
  15. Edwin Brenn
  16. Graham Hyslop
  17. Jadili faida na hasara ya vipengele vya kimajaribio katika kuchunguza dhamira kwenye kazi za fasihi ya kiswahili.
  18. Plato na Aristotle waliweka msingi katika uundaji wa kazi za kisana. Jadili uzuri na ubaya wa misingi hiyo katika kujadili dhamira ndani ya kazi za fasihi ya Kiswahili.
  19. Kujadili dhamira za kifasihi kistoria kuna hasara kubwa zaidi ukilinganisha na faida nyingi tuzipatazo pindi tunapojadili dhamira za kifasihi kwa mtindo mwingine. Tumia mifano lukuki kueleza ukweli wa hoja hii.
  20. Riwaya ya Bwana Muyombekere na Bibi Bugonoka ni miongoni mwa riwaya za Kiswahili za mwanzo kabisa. Jadili dhamira na ufundi unaojitokeza katika riwaya hii.
  21. Maisha ni nini? Wanafalsafa katika fasihi ya Kiswahili wanatoa majibu gani juu ya swali hili?. Je,majibu yao yanakidhi matakwa ya kidhamira enzi hizi za sayansi na teknolojia? Uwanja ni wenu kutoa mifano kun‘tu.
  22. Chunguzeni jinsi Epistemolojia katika fasihi ya Kiswahili inavyokinzana kimaudhui kati ya enzi kabla ya uhuru na baada ya uhuru.
  23. Miaka ya 1970 nadharia ya unegritudi ilitumika sana kuhakiki dhamira katika kazi za kifasihi. Muwe huru kutumia mifano mtakavyo kuthibitisha ukweli wa hoja hiyo.
  24. “Mlimbua nchi ni Mwananchi.” Katika kujadili dhamira za fasihi ya Kiswahili kihistoria methali hii imejipambanua vipi?
  25. “Vipera vya semi vimetumiwa sana na waandishi wa fasihi ya Kiswahili katika kujadili dhamira kihistoria.” Tumia Kiswahili na Malenga na Haki ya Mtu Haipotei kukanusha au kuunga mkono kauli hii.
  26. Huku ukitumia mifano ya kazi za kifasihi, hakiki mabadiliko ya kihistoria kidhamira katika vipindi vifuatavyo:
        (a)  Kabla ya ukoloni
        (b) Wakati wa ukoloni
        ©  Baada ya uhuru

      26. “Mashairi ya Bongo Fleva nayo hayapo nyuma katika kudidimiza na kuibua historia mpya ndani ya jamii ya Waswahili.” Hakiki kauli hii kwa kutumia wanamuziki wanne ndani ya Afrika ya Mashariki.