MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - Matumizi sahihi ya maneno katika uandishi

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: Matumizi sahihi ya maneno katika uandishi
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Mbinu za Uandishi Bora
Matumizi sahihi ya maneno katika uandishi. Waandishi wa habari hawana budi kuwa makini wanapoandika kwa kuchagua maneno yaliyo sahihi na sanifu. 
L
Loga/roga :
Maneno yote yana maana moja. Maana yake ni kudhuru kwa uchawi kwa kutumia vifaa aina ya sihiri, hirizi, kago, azima au amali. Hata hivyo neno lililozoeleka zaidi ni roga.
M
Mazishi/Maziko :
Maneno haya yanatokana na shina moja la ‘zika’ lakini yana matumizi tofauti. Maziko ni kitendo cha kuzika maiti.Tunapokwenda mazikoni tunakwenda makaburini kuzika. Tunakwenda kuhudhuria anakozikwa maiti. Mazishi ni matayarisho kabla ya maziko kama kutafuta vifaa, kuchimba kaburi.
Pia baada ya kuzika kuna matanga na ada zake kama ufanyaji wa hesabu zilizotumika. Maziko yana muda maalumu wakati mazishi hayana muda maalumu. Ni matayarisho tu ya kutekeleza kitendo cha kuzika.
Msiba : Jambo au tukio linalomfanya mtu awe na huzuni, kilio k.v. kufiwa
Masurufu/Marupurupu :
Masurufu (Imprest) ni fedha anazopewa mtu aendapo safarini kwa ajili ya matumizi ya huko aendako. Mhusika anaporudi hudaiwa stakabadhi kuonesha fedha hizo alivyozitumia. Marupurupu (Allowance) ni fedha za ziada anazopewa mtu mbali na mshahara wake. Fedha za marupurupu huweza kuwa ni malipo ya ajari (ovataimu) na una mamlaka nazo. Hudawi stakabadhi. Malipo mengine ambayo huhitaji stakabadhi ni posho ya jamala, posho ya kijikimu, posho ya takrima.