MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - CHIMBUKO NA HISTORIA YA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: CHIMBUKO NA HISTORIA YA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Katika nchi nyingi za Afrika fasihi andishi ilianza kuonekana baada ya kuja kwa wageni. Kabla
ya kuja kwa wageni fasihi anndishi haikuwepo Afrika hasa Afrika Mashariki.
Kwa sababu ya fasihi andishi kuwapo hasa Marekani na Ulaya hata kazi za  fasihi andishi zilikuwepo huko. Dhana ya fasihi andishi ilikuwepo hukohuko.
Yapo mambo mbalimbali yaliyosababisha kuibuka kwa fasihi andishi.
SABABU ZA KUIBUKA KWA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILI
1.  Kutokana na tanzu mbalimbali za fasihi simulizi
Hii ni kusema fasihi simulizi ndio mama wa fasihi andishi.
2.  Elimu rasmi
Katika jamii za jadi za kiafrika hakukuwa na elimu
rasmi. Elimu rasmi ilianza baada ya kuja kwa wageni hasa baada ya ujio wa
Waarabu baada ya wakoloni, hivyo elimu rasmi ilisababisha kuibuka kwa fasihi
andishi.
3.  Kuwapo kwa makazi ya kudumu
Fasihi andishi inahitaji mtu ambaye anakaa sehemu moja
bila kuhamahama. Lakini hapo mwanzo jamii za jadi za kiafrika hazikuwa na
makazi ya kudumu hivyo haikuwa rahisi kwa fasihi andishi kuwapo. Kuwapo kwa
makazi ya kudumu kulifanya wanajamii kuwa na uwezo wa kutulia mahali pamoja kwa
muda mrefu na kufanya kazi mbalimbali za fasihi andishi.
4.      Maingiliano na jamii nyingine
Baada ya kuingiliana kati ya jamii za jadi za kiafrika
na jamii nyingine yaani Waarabu na Waingereza fasihi andishi iliibuka. Mwingiliano
huu ulisaidia Waswahili kupata elimu rasmi, ambayo zaidi ya mambo mengine
iliwafundisha hati za maandishi na mbinu za utunzi na uchambuzi wa kazi za
fasihi andishi.
Kwa hiyo, maingiliano haya yalikuwa na nafasi  muhimu sana katika maendeleo ya fasihi
andishi ya Kiswahili, kwani fasihi andishi ni utamaduni wa kigeni uliotokana na
jamii mbalimbali za Magharibi.
5.      Ugunduzi wa teknolojia mbalimbali
Ugunduzi wa teknolojia mbalimbali ulisaidia sana
kuzifanya tanzu mbalimbali za fasihi simulizi kuvyaza tanzu mbalimbali za
fasihi andishi. Miongoni mwa ugunduzi huo wa kiteknolojia ni ugunduzi wa hati
za maandishi, ugunduzi wa teknolojia ya utengenezaji karatasi na pia ugunduzi
wa teknolojia ya urudufishaji.
6.      Ukuaji wa kiuchumi
Ili uweze kuzalisha fasihi andishi lazima mtu uwe na
uwezo mzuri kiuchumi mfano katika kuchapisha vitabu mbalimbali.
Pia hata hadhira lazima iwe vizuri kiuchumi ili kuweza
kununua vitabu.
 
Ili pia mtu aweze kusoma kazi za fasihi andishi lazima awe
vizuri kiuchumi hasa katika masuala ya kupata chakula ili aweze kusoma kazi za
fasihi andishi.