MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - UTENDAJI SIMULIZI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: UTENDAJI SIMULIZI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Usimulizi wa Hadithi katika Afrika
Okpewho anajadili usimulizi wa hadithi
katika Afrika. Anaeleza kuwa msimulizi wa kijadi ni tofauti na msimulizi
anayepatikana katika maandishi. Usimulizi katika Afrika unafanyika wakati
maalumu hasa wakati wa jioni au usiku watu wanapokuwa katika mapumziko baada ya
vipindi maalumu vya kazi.
Usimulizi wa hadithi katika Afrika hufuata
fomula maalumu. Usimulizi wa hadithi hizi huwa na mianzo na miisho ya kifomula
ingawa mianzo na miisho hiyo hutofautiana toka jamii moja hadi nyingine. Kwa
mfano matumizi ya paukwa pakawa, hadithi hadithi n k kutegemeana na utanzu
husika.
 Pia usimulizi wa hadithi unaambatana
na ushiriki wa hadhira ambaye huonyesha kuwa anafuatilia simulizi hiyo.
Kwa jumla, utambaji wa hadithi jukwaani huwa na
sifa kadhaa zinazoutambulisha. Sifa hizi huzitenga hadithi za mapokeo na zile
tunazozisoma vitabuni.  Utendaji huu unaandamana na sifa zifuatazo;
1.
Usemi
halisi. msemaji anasema moja kwa moja
2.
Michepuko:
msimuliaji hutoa kauli za pembeni au maoni yake. Anaiacha hadithi na kusema
mambo ya pembeni au kando kabla ya kuendelea tena kuisimulia. Michepuko hii
inaweza kuwa na jukumu la viliwazo hasa katika hadithi za kusikitisha au za
kitanzia.
3.     Urudiaji
4.
Matumizi
ya wakati uliopo kihistoria/ au uliopita kisimulizi. Utambaji au usimulizi huwa
katika wakati uliopita lakini huchanganya pia na sifa zinazohusishwa na wakati
uliopo ili kuhakikisha kuwa umbali uliopo kati ya hadhira na hadithi yenyewe
umepunguzwa.
5.
Kubadilisha
muundo wa hadithi: mtambaji anauwezo wa kuubadilisha muundo wa hadithi kwa
kuongeza vitushi fulani, kurudia visa fulani, kubadilisha msamiati, kurahisisha
kisa, kutia ucheshi n.k. Kwa hakika kila utambaji hadithi moja huwa ni tofauti
na utambaji wa hadithi hiyo wa mwanzoni yaani inafaraguliwa.