MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (5)

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (5)
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Kwa kutumia mbinu ya majibizano kati ya mtambaji na mlevi, mwandishi ametumia [i]kilima[/i] kama kejeli kwa viongozi. Kwa
mfano, ametumia kilima cha Magharibi, mashariki, kati na Kaskazini. Dhana hii
inaonesha chuki waliyonayo wananchi kutokana na mambo yanayofanywa na viongozi.
Hii imeonekana dhahiri katika ukurasa wa arubaini na tano hadi ule wa arubaini
na sita, mwandishi anadhihirisha haya pale Mwanahego anaposema:

Asiyefanya
kazi wewe uliye juu ya kilima. Juu ya kilima kuna mashamba? (…) kama kuzalisha
mali ni kusema, kwa maneno yako tungeunda ndege. Basi niache Mwanahego niseme…
Tamthilia
hii inatuonesha jinsi hali ngumu ya uchumi inayopelekea kupanda kwa bei za
bidhaa na kwa baadhi ya mazao ya wakulima kukosa soko, hata inafikia hatua ya
wakulima kung’oa mazao yao ya biashara. Penina (1984) anaonyesha viongozi
wanavyohimiza kuzalishwa kwa mazao hayo ili waweze kufaidi wao wenyewe.
Ameonesha jinsi ambavyo wakulima wasivyofaidi vema faida itokanayo na mazao
hayo. Mwishoni tunaoneshwa jinsi wakulima wanavyoonekana kukata tamaa, katika
ukurasa wa arubaini na sita:
Tunasikia
kuna watu hawataki kulima Wanang’oa kahawa, wanang’oa chai, Taifa linategemea
mazao hayo kupatia fedha za kigeni…
Maneno
hayo yanasemwa na kiongozi, kwa kutumia mhusika Sauti. Mwandishi amemtumia
Mlevi Mwanahego katika kukejeli mambo yanayofanywa na viongozi na kuonesha wazi
jamii inakokwenda na ilikotoka.
Katika
kipindi hiki cha miaka themanini, Tanzania ilikumbwa na janga kubwa la njaa.
Hali ya maisha kwa tabaka la chini ilikuwa ya kutisha. Hali hii ya kutisha
ilitokana na tamaa ya viongozi kujilimbikizia mali na kuhujumu njia kuu za
uchumi. Maisha katika kipindi hiki yalifanana na yale ya kipindi cha Ukoloni ,
na hata pengine kuzidi ya kipindi cha Ukoloni. Katika kipindi hiki, fasihi ya
Kiswahili ilisawiri jamii husika kulingana na matukio na mabadiliko
yaliyojitokeza.
Anatumia
nafasi hii kuwakejeli viongozi waliokuwa wakijilimbikizia mali zao kwa wizi,
uporaji na unyang’anyi na huku wakiwakamata wanajamii kama wezi, mafisadi na
wahujumu wa uchumi. Ametutumia kejeli kuonesha kwamba sio wote waliokuwa wazuri
kwa wakati huo.
Mvungi
(1995) katika [i]Mashairi ya Chekacheka[/i],
ametumia kejeli katika kuonyesha yale yaliojitokeza katika kipindi hiki hadi
miaka ya tisini ambapo kulianzishwa mfumo wa vyama vingi. Mvungi ametumia jina
la kitabu [i]Chekacheka[/i] na baadhi ya
vichwa vya mashairi yake katika kukejeli hali halisi ilivyokuwa katika jamii.
Hivyo basi mbinu hii imemwezesha kwa kiasi kikubwa katika kugusa hisia za
wasomaji na kufikisha ujumbe kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kwa mfano, katika shairi la [i]Utu Umekua Kima[/i]
ukurasa wa kumi na nane, mwandishi anafichua wazi matendo ya viongozi walio
katika tabaka la juu wanavyotumia mabavu yao katika kudhulumu na kuwanyonya
tabaka la chini.
Mvungi
amewakejeli wale viongozi wa vyama mbalimbali ambao hujifanya wenye kuwaagiza
walio chini yao kwa kuwalipa ujira mdogo huku waking’ang’ania wakidhani ndiyo
hekima. Tabaka la chini hapa linachekelewa kwa kukejeliwa kuwa hata wakisemwa
namna gani wasiache kutumika. Waendelee tu.
Wakati
mwingine, Mvungi amekuwa akionesha wazi maisha yalivyorudi nyuma kwenye kipindi
cha utumwa. Kwa mfano, katika shairi la [i]Utumwa
Uhuru
[/i] ukurasa wa ishirini na mbili, anaonesha kukosekana kwa demokrasia
baada ya uhuru kupatikana. Bado viongozi wameshikilia enzi za Ukoloni, kichwa
cha shairi hili ni kejeli juu ya uhuru na uongozi wa nchi za Kiafrika. Katika
ubeti wa tatu tunasoma haya:
Pili
ni utumwa huru, Afrika ilobaki
Matabaka
yanadhuru, raia hawana haki
Ni
maisha kwa ushuru, maisha ya shakishaki
Maisha
yenye utupu, watu roho mikononi
Mwandishi
anaonesha kukosekana kwa haki na demokrasia inayotokana na utawala wa chama
kimoja. Katika shairi hili mwandishi anakejeli siasa ya nchi ambayo chama
kimoja kinatawala. Hali hii hairuhusu demokrasia kwa wananchi kwani kila
lisemwalo huwa ni sawa tu bila maamuzi ya wengi.
Vilevile
katika shairi la [i]Gunia la Mikutano[/i]
ukurasa wa ishirini na tano, mwandishi anakejeli uongozi uliokithiri kwa
unyonyaji, ulaghai, unyanyasaji na rushwa. Viongozi wamekuwa watu wa maneno tu
na ziara ambazo huhitaji michango kutoka kwa wananchi. Ametumia neno [i]gunia[/i] kukejeli mikutano na ziara nyingi
wanazofanya viongozi huku wananchi wakiambulia patupu. Haya yanadhihirishwa
katika ubeti wa tatu:
Gunia
la mikutano, pipa la maandamano
Hotuba
kwa mashindano, kazi kubwa ni maneno
Michezo
na michuano, haya ya mshikamano
Matokeo
ni mateso, na kutojali shida.
Hali
kadhalika katika kufichua mfumo mzima wa uongozi mbaya katika jamii mwandishi
Mvungi ametumia kejeli kwa vichwa vya baadhi ya mashairi yake. Kwa mfano,
shairi la [i]Chanzo cha Huo Uozo[/i] ukurasa
wa ishirini na nne, [i]Ulanguzi Umevaa Suti[/i]
urasa wa kumi na tano; na [i]Mtoto Aso
Riziki
[/i] urasa wa ishirini na sita, n.k. Katika mashairi hayo mwandishi
anaonesha rushwa iliyokithiri katika jamii ulaghai wa kisiasa, urasimu na
matumizi mabaya ya mali ya umma. Hivyo basi mwandishi Mvungi katika diwani zake
za [i]Mashairi ya Chekacheka[/i] (1995), [i]Raha Karaha[/i] (1978), na [i]Chungu Tamu[/i] (1985) ametumia kejeli
katika kufichua uozo uliopo katika jamii. Mwandishi ametumia mbinu hii kuonesha
hali ya maisha, demokrasia, utabaka na uongozi mbaya. Hivyo basi mbinu hii
imemuwezesha kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kwa kazi zake kifani na kimaudhui.
Pamoja
na fasihi ya Kiswahili kutumia kejeli kusawiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa
kiuchumi na kisiasa kwa kuzingatia mabadiliko na matukio mbalimbali katika
jamii; kejeli katika jamii hutumika katika kusawiri duara la maisha ya binadamu
kwa kuwa kuna kupanda na kushuka na pia huwa na mwanzo na mwisho.
Kezilahabi
(1988) katika [i]Karibu Ndani[/i] ametumia
dhana ya [i]chai[/i] kuonesha mzunguko wa
maisha ya binadamu kwamba ni duara hivyo hatuna budi kufanya yaliyo ya
mafanikio wakati wa maisha yetu kwani mwisho wa maisha upo.
Katika
shairi la [i]Chai ya Jioni[/i] ukurasa wa
tatu, ubeti wa kwanza tunasoma:
Wakati
tunywapo chai hapa upenuni
Na
kuwatazama watoto wetu
Wakicheza
bembea kwa furaha
Tujue
kamba ya bembea yetu
Imeshalika
na imeanza kuoza
Na
bado kidogo tutaporomoka
Katika
shairi hili mwandishi amezungumzia maisha ya viongozi walioko madarakani.
Anaonesha wazi jinsi viongozi wanavyofaidi wakiwa madarakani lakini pindi
wang’atukapo hurudi katika hali ya kawaida. Hivyo anawakejeli kwa [i]chai ya jioni[/i] akiwakumbusha kuwa
wasijisahau kuwa ipo siku watayarudia maisha yaliyo sawa na ya wanajamii
wengine. Haya yanadhihirishwa katika ubeti wa mwisho wa shairi:
Lakini
kabla hatujaondoka kimyakimya
kukamilika
nusu duara iliyobakia
tuhakikishe
vyombo vyetu ni safi
Hapa
tunaona kwamba, pamoja na mwandishi kutumia kejeli katika kuonesha mfumo mzima
wa maisha na uongozi, mwandishi ametumia pia mbinu hii katika kuonesha
mabadiliko na mgogoro wa ushairi uliotokea miaka ya sabini.
Katika
shairi la [i]Karibu Ndani[/i] ukurasa wa
thelathini na nne hadi ule wa thelathini na saba, mwandishi anazidi kukejeli
mgogoro wa ushairi wa kimapokeo. Shairi hili la Karibu Ndani ni mwendelezo wa
shairi la [i]Fungueni Mlango[/i] lililo
katika diwani ya [i]Kichomi[/i]. Katika
mashairi haya yote msomaji anakaribishwa ndani ajionee ushairi wa kisasa.
Katika
sehemu ya kwanza ya shairi la [i]Karibu
Ndani
[/i] mwandishi anaukejeli ushairi wa kimapokeo kwa kuufananisha na kibanda
kikuukuu ambacho kinakaribia kuanguka, akimaanisha kuwa ushairi mapokeo hauna
nafasi wakati huu, kwani muda si mrefu utakuwa umekwishapoteza watunzi pamoja
na wasomaji wake.
Washairi
wa mapokeo, sasa wacheza lala salama
katika
mionzi hafifu, ya jua machweoni
Tunaona
jinsi mwandishi anavyowakejeli wale walioshikilia mashairi ya kimapokeo
waingie. Anawashauri katika mashairi ya kisasa yasiojali urari wa vina na
mizani bali kuzingatia zaidi fani na maudhui. Hivyo basi mwandishi anahimiza
washairi hao waende na wakati na kuacha mapokeo ushairi yaliyoigwa kutoka Ulaya
na kufuata yale ya Kiafrika. Haya yapo katika ubeti huu wa pili:
Muda
si mrefu patakuwa kiza tororo.
Kwenye
kiza cha karne pasipo vichochoro mkato
nilikuwa
na nanga yangu, nyimbo mpya natongoa
Mwisho
ukurasa wa thelathini na moja, mwandishi ameukejeli ushairi huo kwa kuulinganisha
na mbwa aliyezeeka na asiye na meno aitwaye Mavina:
Nje
kulikuwa na mwanga, nao ndege wakiimba
Kulikuwa
na njia katikati, wanyama kila upande
Walioinamisha
vichwa, kati nilipopita
Nilipouacha
msitu, nyuma nilitazama
Mbali
nilimwona Mavina, akitangatanga msituni
 
Mwandishi
anatuonyesha kupotea kwa Mavina ambapo hawezi kugundua wala kubahatisha njia ya
kurudi alikotoka. Anaukejeli ushairi wa kimapokeo kwa kuuashiria kupotea kabisa
kwa sababu hauna mashiko na umepwaya.