MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: KALAMU YANGU

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: KALAMU YANGU
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
KALAMU YANGU
heko nakupa kalamu, unayenipa kunena,
Ninaposhikwa na hamu, jambo moja kulinena,
Wala sipati ugumu, madhali ninavyo vina,
Ni wewe waniauni, Asante sana kalamu.

Bila wewe singekuwa, na vile sauti sina,
Na waja ningezomewa, wabaki kunitukana,
Lione limepagawa, waja wangesemezana,
Sasa wanipa heshima, Asante sana kalamu.

Fulani bin fulani, naye leo twajuana,
Kunitia masifuni, eti ninajua sana,
Ningekwea jukwaani, niseme najua sana,
Nani angeniamini, Rafiki yangu kalamu?

Neno hili liafiki, Wala tusingejuana,
Wangesema hatutaki, maneno kurushiana,
Kalamu si mnafiki, Mimi nawe twapendana,
Mbali umenipeleka, Asante sana kalamu.

Ofisini nilipita, pengine wangeniona,
Kikumbo wakanipita, mithili wajaniona,
Wangu moyo ulipwita, Cha kufanya ndio Sina,
Libaki kugugumia, hali mpweke kalamu.

Ndipo ukaniambia, andika watakuona,
Na hapo nikaamua, kuandika kikazana,
Ingawa sijatoboa, ninawaza mbali sana,
Popote niende nawe, mwendani wangu kalamu.

Wengine huniuliza, yu wapi huyu kijana,
Ni binti ama ajuza, wanataka kuniona,
Pengine huwashangaza, hivi nivyo msichana,
Wanabaki bumbuwazi, lijue hili kalamu.

Kalamu kipenzi changu, wa ubani maridhia,
Wanipa raha mwenzangu, vile ninakutumia,
Wala hunipi machungu, kwangu huzuni kuzua,
Daima tutabakia, Mimi na wewe kalamu.

Nitapofika ajuza, hapo macho hayaoni,
Kalamu tanitangaza, na kunitia thamani,
Huko utanieleza, Ulaya na Marikani,
Tafadhali niamini, tanikumbuka kalamu.

Wengi tunao galacha, waandishi maarufu,
Tayari wametuacha, weshaenda kwa Raufu,
Maandiko kuyaacha, jambo lenye utukufu,
Mfano huyu Shabani, humkumbuki Kalamu?

Afiki Mimi na wewe, tumezidi pete chanda,
hivi wanipa kiwewe, kalamu umenishinda,
Kama mtu na mkewe, nakupenda wanipenda,
Mwisho wa kutumbuiza, nakuheshimu kalamu.


Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704