MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: KAZI YA NANI MALEZI?

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: KAZI YA NANI MALEZI?
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
KAZI YA NANI MALEZI?

Baba:

Baba nipo kataani, sikubali jambo hili,
Hanifiki akilini, kwani sioni halali,
Mtoto alee nani, baba! Hilo sikubali,
Kazi ya mama malezi, baba natafuta mali.

Mama:

Bwana ungebadilika, zetu enzi sio zile,
Tena ufanye haraka, utaaibika mbele,
hicho unachotamka, nakucheka ni ukale,
Zimebadilika zama, malezi mama na baba.

Baba:

Shule imekuharibu, mwanamke kaa chini,
Umeishiwa adabu, hiyo ni tabia gani?
Mie na zangu sharubu, huyo mwana tampani?
Kazi ya mama malezi, baba natafuta mali.

Mama:

Ishushe yako sauti, taamsha majirani,
Ukujalie umati, katikati ya manani,
Wanitupia kijiti, nilee peke kwa nini,
Zimebadilika zama, malezi mama na baba.

Baba:

Umeanza mazoea, kielimu uchopata,
Ujue nakushangaa, mama uache Matata,
Nani unamtupia, hiyo kazi ulopata?
Kazi ya mama malezi, baba natafuta mali.

Mama:

Wajua kazi malezi, au bure unafoka?
Kikwachia hauwezi, majasho yatakutoka,
Tofauti chini weka, tufanye sote malezi,
Zimebadilika zama, malezi mama na baba.

Baba:

Hebu tia umuhimu, hicho witacho malezi,
Bure unanilaumu, ninaona ni upuzi,
Hakinipi utimamu, wawili kwa moja kazi,
Kazi ya mama malezi, baba natafuta mali.