MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: KITU GANI USHAIRI?

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: KITU GANI USHAIRI?
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
KITU GANI USHAIRI?

Amri Abedi 1954: 

Shairi ama utenzi, Mimi naona ni wimbo,
Lisoimbwa sijiponzi, hilo kulitia nembo,
Nikaanza kukienzi, kitu kichokosa umbo,
Ni shariti kuimbika, hapo taita shairi.

Shaaban Robert 1958:

Tena sanaa ya vina, tenzi nyimbo na shairi,
Maneno si mengi sana, fasaha yasiyo shari,
Shairi wimbo mpana, Wimbo ni dogo shairi,
Lililopea shairi, hilo twaita utenzi.

Naendelea Shabani, kueleza waziwazi,
Mwasema vina nini? Kufasili hamuwezi,
Sauti zilolingani, mfano silabi zi,
ziwe sare utungoni, hapo twaviita vina.

Mathias Mnyampala 1965:

Ni maneno ya hekima, tangu kale tungo hizi,
Cha thamani na heshima, Mfano wake feruzi,
Mwanadamu huyafuma, ya dunia maongozi,
Kwa maneno ya mkato, huyanena ya moyoni.

Jumanne Mayoka
1986:

Wa kisanaa utungo, mpangowe maalumu,
Wenye vina kwenye kingo, na mizani ilo timu,
Shairi haliwi chongo, zote pande ni muhimu,
Za fani na maudhui, manenoye kwa mkato.

Euphrase Kezilahabi 1973:

Ukale napiga teke, fikira zenu hafifu,
Kuzitaja sifa zake, Mimi naona dhaifu,
Sheria ni kitu teke, kinaleta usumbufu,
Sasa naleta usasa, nazivunja desturi.

Ni tukio ushairi, pia hali au wazo,
Lenye mpango mzuri, na mizani mzomzo,
Ufasaha sio shari, lugha iliyoliwazo,
Na ueleze ukweli, maisha ya binadamu.

Mulokozi na Kahigi 1973:

Ni mpango maalumu, wa fasaha na muwala,
Lenye mafunzo muhimu, liso funzo hilo wala,
lihusulo binadamu, yale ya lila na fila,
hisia ziguse moyo, yawe mahadhi ya wimbo.

Mtunzi:

Ulikuwa ubishani, ni kitu gani shairi,
Japo kidogo zamani, naona zake athari,
Husema vina vya nini? Wengine huleta shari.

Naleta yangu mawazo, nionavyo mie Sanga,
Shairi sio mchezo, sema unatungatunga,
Wala sio maelezo, uanze kuyabolonga,
Wala hatutungi shanga, shairi lina kanuni.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704