MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - Eleza tofauti kati ya hadhira ya fasihi andishi na fasihi simulizi

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: Eleza tofauti kati ya hadhira ya fasihi andishi na fasihi simulizi
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
a)Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na fanani ilhali ile ya fasihi andishi sio lazima iwasiliane na mwandishi.
b)Hadhira huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi k.v kwa kuimba, kupiga makofi n.k (hadhira tendi/hai) ilhali hadhira ya fasihi andishi haichangii katika uandishi.
c)Hadhira ya fasihi simulizi huonana na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi andishi si lazima ionane na mwandishi.
d)Hadhira ya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ile ya fasihi andishi kwani huhusisha hata wasiojua kusoma na kuandika.
e)Hadhira ya fasihi simulizi ni hai yaani inajulikana na fanani ilhali ile ya fasihi andishi si hai yaani haijulikani na mwandishi.
f)Hadhira ya fasihi simulizi hainunui kazi ilhali ile ya fasihi andishi hununua kazi.
g)Hadhira ya fasihi simulizi yaweza kumiliki kazi ya fanani lakini ile ya fasihi andishi haiwezi kumiliki kazi ya mwandishi.
h)Hadhira ya fasihi simulizi huchagua kwa kulenga watu wa rika fulani lakini ile ya fasihi andishi hailengi watu wa rika yoyote.